Monday, July 29, 2013

Stellah Mathias Mosha Pre Wedding Party...Classy!

Huku akizungukwa na mashosti wake wa A'Level, paleee Green Acres, akiwamo Winnie na Vanessa, mrembo huyo mwenye asili ya Kiraracha- Moshi, Bibi Stellah mwana wa Mosha,,aliingia ukumbini pale- King Palace, Sinza- kwa tabasaaam la ukweli na huku akishangiliwa kwa vifijo, nderemo na hoihoi kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki.

Akasindikizwa na kazi nzuri ya Christina Shusho, Nipe Macho Nionee, Bi arusi huyo akasogea na kumleta mbele ya kadamnasi na kumtambulisha rasmi mumewe mtarajiwa, Bw Nixon Biharabu. Kama vile haitoshi, Stellah akampatia zawadi mmewe yule mtarajiwa ya saa ya mkononi na kumvisha kimahaba. That was a thing!

Crew ya McNdimbo ikaja na ladha tofauti, ikiwa na ushiriano wa karibu na sound iliyokwenda shule kutoka kwao Kwayu Entertainment chini ya Dj Danny. Moto ulikua ni wa hataree wa muziki ule.

Katika kuleta uhondo wa kutosha, JJB Smart Boys wakachombeza na show yao safi ya Zunguka.
Kwa kweli, ile ilikua so goood of a special Night ya Stellah Mosha.

Songa nasi kwa picha hapa

Colours: Red na Gold



Friday, July 26, 2013

Bw na Bi Kajenje get Married...

Katika kile kilichoonekana kama crew ya McNdimbo Entertainment basi itafunga kazi mwaka huu kwa kufanya shughuli zilizoongozana hapo katika ukumbi wa The Best Choice, Bw na Bi Kajenje walionekana kufungua pazia la mfululizo huo. Mara baada ya kuuacha ukapera, Bw Kajenje akiingia na mkewe ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili, walipata chaguo la wimbo mzuri kutoka kwa Bi harusi katika album yake mpya.



Kamati ya ulinzi ikiongozwa na mwanataaluma Emmanuel Kihongo na mdau katika sekta ya uvuvi na rasilimali za majini, Bw Humphrey Mahudi, ilisimama kidete kuhakikisha hakuna mtu anaingia pasipo tiketi ya siku hiyo ambayo ilikua ni kadi.



Ukumbi ukiwa umepambwa na kupambika ukawa na wageni waliochangamka ile mbaya, ukawekwa katikati ya burudiko la moyo kutoka katika crew yenye kuthamini burudani, McNdimbo Entertaimenment...Your Satisfaction is our Passion.



Songa nasi kwa picha hapa.



Colours; red na yellow



Edwin Msambwa weds Agnes....what a Handsome Couple!

Katika kile kilichoonekana ni kampeni madhubuti inayoratibiwa kitaalamu haswaaa ya kuhakikisha vijana wote wa Idara ya Lugha za Kigeni na Isimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanapata wenzi wao wa maisha, sasa ikawa zamu na Mhadhiri Msaidizi Bw Edwin Msambwa pale alipofunga pingu za maisha na Bi Agnes.

Wakiwa na asili ya Nyanda za Juu Kusini; Njombe na Iringa Mjini, maharusi hao wakaingia ndani ya Ukumbi Murua wa Five Star kule Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Kwakua wote ni wapenzi wa Kwaito haswaaaa, basi wakaingia wakijimwayamwaya na buudani safi kutoka Afrika ya Kusini na bila ajizi Dj Smol akawaunganisha na mijikwaito ya haja.

Huku wakisindikizwa na wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi kutoka pale Nyerere Campus almaarufu kama Mlimani; Mwombeki, Njiro, Abel, Peji, Faraja na wengineo, wakajikuta wakitabasamu kuanzia mwanzo wa shughuli mpaka mwisho. Zaidi wakawepo wanataaluma wabobevu kuhakikisha wanakuwa mashuhuda wa tukio lile muhimu; Prof Rugemalira, Dr Kibogoya, Dr Muzale, Dr Mapunda na Dr Upor ambaye pamoja na kwamba alikua safarini siku hiyo alihakikisha hapitwi na tukio hilo mara tu baada ya kuwasili jijini.

Burudani mdio jafi yetu na watu ndio haswaa furaha yetu kuwapa burudani...

Songa nasi hapa

Colours; red na gold na green



Tuesday, July 16, 2013

John Weds Domina...A lovely Couple!!!!

Wakiwa na nyuso za furaha na tabasamu zao za asili kabisaaaa..wamefanana kimtindo ka mapacha wa mbali hivi, marafiki wa kitambo hao; John Augustino Gachinya na Domina Damian Mkangara wakaingia na shangwe za haaja katika ukumbi maridaaadi; The Best Choice pale Tabata Aroma, Dar es Salaam!

Ikiwa pia si siku maalum ya Bi Harusi, Domina, ambapo ilikua pia ni Birthday yake. Kwa ujasiri na upendo wake kwa mmewe huyo, bi harusi akakata keki yake kwanza na kumlisha mumewe huyo. Baadaye akawalisha wazazi wake na kufuatiwa na keki ya harusi.

Nderemo na hoi hoi zikafurumuka kutoka kwa wanyarwanda wale na wanyakyusa. Hapo ikawa ileee mambo ya kunyanyua na kutawanya mikono na huku miguu ikishtua namna hii...yaaani. Kwa ukaribu kabisa maharusi hao, ambao walifunga ndoa hiyo pale St Peters, wakasindikizwa na mabesti zao wa ukweli;Mr Mathias na Mkewe, Theresia wana wa Mbogoni.

Dada wa Bwana harusi, Mrs Pierita Shariff, akapewa shavu dodo na marafiki zake wa ofisini kwao, Wizara ya Mambo ya Ndani; Saburi a.k.a Mamaa Mc, Asha wa Asante na mmewe Nyamiela, Imani, Happy Mkwe, Jamali, Halima Mzungu, Ruanda, Hamida, Violet Mamaa wa Upako, Kuruthum, Agatha na wengineo.

Haikua taabu kwa Mtaaluma wa Burudani kuikosha hadhira ile, pamoja na kwamba shughuli ilichelewa kuanza kufuatia kukamilika kwa mambo ya protokali. Uhondo siomwa kulazimisha, ni NATURALLY!

Passion yetu ni kukuwezesha mteja wetu kupata burudiko la moyo....

Songa nasi kwa picha

Colours; Black,Silver na Red













































































HAAAAPI BIRTHDAY TO UUUU!!!!












Mathis na Kipenzi Chake, Theresia