Sunday, September 29, 2013

Gasto Mwakilasa Weds Ngajabule Mwasikili...

Wakiwa na nyuso zilizokolezwa na tabasamu la ukweli kabisa, Bw Gasto Mwakilasa na mkewe Ngajabule Mwasikili waliingia ndani ya Ukumbi mpya wa Mbuji hapo jijini Dar es salaam. Huku wakisindikizwa na Marafiki zao Bw Lumuli na mkewe Mpoki, maharusi hao walionesha kua ni marafiki walioshibana siku nyingi. Hapo walikua wanatokea KKKT Ubungo
 
Burudani ilikua ni ya hatariii, Dj Smol akiwa nyuma ya mashine na mdau akichombeza kwa ukaribu, wanyakyusa wale wote kutoka wilaya ya Rungwe, Mbeya walikua wamekunika ile hatari!! vitu vya Naloliiii...tummogeleee...ndaaga...eeena!! weee...gospoooz...bak-2-bak na misebene ya kukata na shoka na taarabuuz,,,basi weee.
 
WE REALLY AMAZED OUR CUSTOMERS!!
 
Songa nasi kwa picha hapa.
 
Colors: Purple na Baby Yellow
 
 
 
 

Wednesday, September 25, 2013

Filbert Kinunda Weds Cellina Muhe...... @ Mbezi Garden Hotels

Raha ya wamatengo, wacheze n kufuraahi...basi hapo tabasamu kwa sura na mioyo yao halikauki. Hapa ilikua siku maalum kabisa kwa Bw Filbert Kinunda kutoka kuleee Mbinga na Bi Celina Muhe mwenye asili ya Wairaki kutoka mkoa wa Arusha. Hawakua na sababu ya kutoamini yale yalioandikwa...wakawaacha baba na mama zao, wakajongea madhabahu ya Kanisa la Elshaddai Temple International na kuambatana rasmi wakiwa Mr & Mrs Filbert Kinunda. Maharusi hao walisindikizwa na marafiki zao wa siku nyingi; Bw na Bi Davis Nyanda.
 Burudani safi kutoka kwa Kwayu Music Classic chini ya Dj Danny na uhondo wa Mdau hapa, shughuli safi ile ndani ya ukumbi murua wa Mbezi Garden Hotels ikageuka ni ukumbi wa burudani na huku tukipata maneno ya busara kutoka kwa Mchungaji Kinunda na wakwe.
Songesha hapa kwa uhondo zaidi
Colours; Baby yellow, black na purple



Wednesday, September 18, 2013

William Kaposwe Weds Maria M'bade....Picolo Beach Hotel

Ukumbi ukiwa na nyuzi joto chache za kuwezesha waalikwa kujisikia kma wako nje ya jiji la Dar es Salaam, pembezoni mwa bahari ya Hindi... uwepo wa Mungu ukijidhihirisha na kuwapa faraja maharusi hao; Bw William Kaposwe na kipenzi chake Maria,wakafunga pingu za maisha pale Nayoth Church na kujimwaga hapo Grand Hall-Picolo Beach Hotel. Wakisindikizwa na marafki zao wa ukweli Bw Allen na mkewe Victoria, wana wa Mwandosya.

Kazi nzuri na burudani ya muziki ikidondoshwa na Respect Djs, chini ya utaalam wake Dj Pimbi ikawaweka katika kilele cha burudani wageni na familia zile. Kwa kuheshimu imani ya maharusi, familia na wageni wale, crew yetu ya burudani ikagawa full gospel style mwanzo mpaka mwisho wa sherehe ikwa na exceptions kidogo katika mtoko halisi wa kwaito.

Hakika burudani ilifika mahali pake...hii ndo raaaha ya McNdimbo Crew ktika kuhakikisha slogan yetu yafikiwa na kuboreshwa kila kukicha; YOUR SATISFACTION IS OUR PASSION!

Songa kwa picha hapa...

Colours: Aqua Green, Hot Pink na Baby Yellow

 


Monday, September 16, 2013

Bi Harusi na Vidani....Chains za Gold?

Bridal Jewelry Ideas
        
Wapendelea big bold bling or more subtle jewelry? Ngoja nikudokeze (kwa msaada wa internet sources) what to wear and how to wear it. Angalia the right wedding jewellery for your big day and walk up the aisle in style.
It might seem as all jewelry that matters on the big day is the wedding rings, but there's a lot more to consider when it comes to choosing bridal jewellery. Choose pieces that flatter you and the dress. It's important to spend some time considering what you want and whether it matches with the elements of your bridal 'look'.

Wedding Ceremony Flowers & Decorations

Wedding Ceremony Flowers & Decorations
What's a wedding reception without stunning flowers and great decorations? hapa natupia maujanja kidogo to help you create the most beautiful wedding ceremony.
A wedding ceremony wouldn't be the same without well thought out decorations and flowers. Whether it's a scattering of lilies in winter or bright yellow daffodils in springtime they all have their place and you when it comes to your big day you will need to decide on the flowers you want. You could also add candles, drapes and balloons to complete the look.

Friday, September 13, 2013

Friday, September 6, 2013

Here!! Deus Kapinga weds Juliet Malibate...wow!!

Hukuwahi kuona wamatengo wakiwa wamechangamka asee...Yaani It was so difficult to imagine wakerewe wanaweza kuleta mixture ya hatari katika burudani na kuwezesha high table iwe na tabasamu za hatari kutoka kwa wanandoa wapya kabisaaa; Bw Deus Cletus Kapinga na best friend wake na mkewe mrembo haswaa, Bi Juliet Malibate. Hapo ilikua ni mshikemshike mwanzo hadi mwisho wa kaaazi.

Wakiwa na marafiki zao wa karibu, Benitho na Angela-mkewe na maids walio na mtoko wa rangi mchanganyiko hapo baaasi...kuangalia huku wakutana na gromm's men wakiwa na suti zao nyeusi na tai zenye mchanganyiko wa crazy colours...ilikua ni mkusanyiko wa watanashati na warembo haswaaa.

wakaingia kwa mbwembwe...wakacheza kwa furaha...wakajiachia kwa raha...wakaserebuka ile mbaya like nobody is watching!! Dj Smol akawapagawisha, wakapagawaaaa...ukumbi ukarindima na kutikiswa na sauti ya biashara kutoka kwa mtaaluma mbobevu mwenye vionjo visivyochosha,,Mwana wa Mshikemshike-McNdimbo!! Weeeee....YOUR SATISFACTION IS OUR PASSION!!

Kimatengo na lindeku la asili kabisaaa...za zamani...za injili na uhondo halisi wa kwaito...halafu kama klabuuuu;;;;;; Tupooogo! na zile Personally!! wataka nini tena hapo...burudani mwanzo-mwisho apo...Furaha ilioje...

Songa nasi kwa picha

Colours; Purple na Pink

Thursday, September 5, 2013

Lourine Jimmy's Fabulous Night...

Cha kwanza waweza kuona pale akitabasamu tu ni uleee mwanya...Mtoto wa Tanga huyo mwenye mwonekano wa kishombeshombe baab..LOURINE JIMMY. Ikafika wakati muafaka hapo ambapo aliamua ka moyo mkunjufu kuwaaga ndgu na jamaa ili akayaanze maisha ya ndoa takatifu na wake wa ukweli.
Wasambaa hao bila kushangaa wakajipanga vilivyo na kuamua kushirikisha ndugu, jamaa na marafiki ili kumuaga kipenzi wao katika ukumbi wa Lukolo, pale Tabata. Huku wakiwa na ucheshi wao wa asili na usongo wa haja wa kuburudika haswaaa na ngoma zao za asili bila ya kusahau maisha ya kiroho ya familia ile na kuburudika kwa nyimbo za injili na kumtukuza BWANA. Bila ajizi, crew nzima ya McNdimbo ikatoa ile raha ya ukweli na asili ya kukonga nyoyo za waalikwa. Hapo ni kata kiu mpaka kufikia malengo; YOUR SATISFACTION IS OUR PASSION....
 
Songa nasi kwa picha ...
 
Colours: Purple na Baby Yellow