Tuesday, December 31, 2013

Maurice Njowoka weds Paulina Msanga @ Sunset-Tembo; Diamond Atumbuiza!!

Wamanda na Wapare!! Yaani hapo shughuli lazima ibambe....mwendo mdundo!! Tuserebukeee aeee aeeee....mara huku...libegho la mwana li hajaaa...aeeee lihajaaa! weee
Maurice Njowoka, Meneja wa Coca Cola Light, akiwa na tabasamu lake asilia akasahau mambo yake ya marketing kwa muda na kumuangalia usoni mtoto wa kipare, mrembo wa asili, Bi Paulina Msanga na kumvisha pete ya dhahabu kidoleni, huku akitamka maneno yatarajiwayo "For bera for worse..." paleeeee RC-Sinza na kutamkwa rasmi kuwa
Mr & Mrs Maurice Edwin Njowoka.
Vigelegele na nderemo za haja vikaanza hapo , huku wamanda wakigalagala chini kuonesha kupendezwa na kukubalika kwa tukio lile la kihistoria. Hapo nje kanisani watu wakacheza Lindeku (ngoma ya watu wa Manda, Songea) na kujiachia haswaaaa.
Shughuli ikahamia paleee Mbezi Beach katika ukumbi maarufu wa Sunset-Tembo Hall. Kumbi likasheheni na kutapika watu takribani 700!! Hapo nyuma ya mashine yupo Dj Ndende kutoka Respect Djs (www.shereheyetu.blogspot.com) na katikati nipo mdau na blogger wenu. Tukawasha moto wa hatareeee. Hiyo ni trelaaa...ikaja ngoma ya mganda na baadaye Jerry Mtumishi akatoa burudani yake.
Ikaja surprise ya kufungia mwaka sasa...kwa mbaaali ikasikika sauti yake "tatizo kwetu mbagalaaaaa..", akaongeza tena '..you are my number one..my swt.." hahahahahaa! Kitu cha Diamond Platnumzzzz!! Watu wakapagawaaaa...yaani ni burudani kwa kwenda mbele!! What else did we have to say? Hii ilikua harusi iliyostahili kufunga mwaka kwa crew nzima ya McNdimbo Entertainment!!
YOUR SATISFACTION IS OUR PASSION
Songa nasi kwa picha
Colours: Aqua Green, Silver na Red

Thursday, December 26, 2013

2014 Wedding Color Of The Year is Radiant Orchid!

                                                                                                                                                                                   
lavender wedding bouquet
Pantone's color of the year huwa in influence kubwa katika fashion, design na weddings. Ingawa hapa Tanzania, many have been shading the purple kwa 2013, imekua kama tumedandia treni kwa mbele but now Tunataraji hii rangi itaonekana katika weddings nyingi in 2014 -- it's lush and sophisticated, and even though pink and purple are often seen as "girlie" colors, ikla hata men wanapendeza nayo tuu. Inapendeza sana hii na inaweza kuwa paired with deep colors like navy blue, eggplant, na olive green. Here are some of our favorite orchid wedding details to inspire you!
Radiant orchid is beautiful in wedding bouquets, inaweza kwenda na all shades of pink and purple




Purple and red modern wedding 9


Tuesday, December 24, 2013

We Wish Our Esteemed Customers Merry X-Mass & Happy New Year!!

 
Tumekua pamoja kwa kipindi chote cha mwaka mzima. Tukifanya kazi pamoja, tukifurahi na tukiwa na wakati mzuri katika sherehe, makongamano, matamasha na shughuli nyinginezo. Ni wakati mzuri wa kuwatakia Heri ya Krismas wateja wetu.
 
 
 
Tumepanga pamoja na kuwa na matarajio mazuri kwa kipindi cha 2013 na sasa tunajongea na kufikia tamati. Tunawaahidi kurekebisha yale yote mliyotushauri tuyarekebishe. Tulikua na tatizo la muziki na kwa sasa tumelikabili kwa 100% katika kipindi cha mwaka 2013. Tumekua na maDJ wenye hadhi na wanaojua wajibu wao. Ni furaha kuona mnatuamini na kutukubali. HERI ya MWAKA MPYA!!
 
 
Tuwe pamoja na tuwe na wakati mzuri katika kipindi hiki kijacho. Tumejipanga vizuri na tunaamini tutakonga nyoyo za watu wengi zaidi kwa kua tunajali mila nadesturi, imani na muda wa shughuli husika.
 
 
YOUR SATISFACTION WILL ALWAYS BE OUR PASSION

Sunday, December 22, 2013

John Mabamba weds Pendo Alex @ Kwalalumpa, Sinza

Pale AIC, Chang'ombe, zikasikika kengele...ikiwa ni siku chache tu kabla ya Kristo kuzaliwa, Mtanashati John Shabani Mabamba akajongea kwa altare na kukutana na rafiki na neighbor wake wa ukweli, Bi Pendo Alex...kwa pamoja wakaapa kuishi pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha. Kiapo hicho kilifuatiwana nderemo na vifijo vya haja haswaaa
 
Wajita wale wakajichanganya na wakwe zao ambao ni wakurya...majirani asilia kutoka kule Mwilingo na Kiagata, Serengeti..wakafurahi kuunganisha undugu. Ni burudani ya haja kutoka kwa HB entertainment wakiwa na Respect Djs (Dj Bruno) na nyuma ya mic akawepo mdau wenu wa kawaida, McNdimbo!! Weee, taka tena kitu gani banaa. Ndani ya Kwalalumpa-Sinza hapo ni Cheza, ruka na jiachie ndo ukawa mpango mzima.
 
Kaka wa Bwana harusi, ambaye pia ni mlezi wake, Bw Moses Mabamba a.k.a Big Mo, akaonesha umahiri wa kulisakata sebene kwa kuweka chupa ya bia kwa kichwa na kujiachia apo akiwa na mpenzi mkewe Bi Witnes na wanao Dorry, Kurwa na Dotto.
 
Songa nasi kwa picha
 
Color Combo: Yellow, Red, Black na Gold
 
 
 
 
 
 

Sunday, December 15, 2013

ELICE MREMA is sent off at KRISTO MFALME in Dar es Salaam...

Akiwa na kumbukumbu za nyumbani, Tanzania, baada ya kuondoka kwa muda wa zaidi ya miaka saba na kwenda kuishi Marekani, Elice Mrema, akarudi na kuja kuagwa rasmi ili apate Baraka za kuolewa na kuishi na kipenzi na rafiki yake wa ukweli, Francis Thairu.
 
Shughuli hiyo ikiwa na muonekano wa kimataifa zaidi, ambapo bwana harusi ana asili ya County ya Kiambuu kwa kijiji cha Kabete karibu kabisa na Nairobi. Huu ni muungano wa haja wa Afrika ya Mashariki.
 
Furaha na nderemo zikasikika hapo ndani ya ukumbi wa Kristo Mfalme hapo Tabata, jiji la Dar es Salaam. Wachagga wakashikana mikono na wakikuyu wakijiachia kwa furaha kabisaa.
 
Crew nzima ya McNdimbo kwa kushirikiana na Respect Djs (www.shereheyetu.blogspot.com) wakawasha moto. Zikapigwa za Kenya na za Tz na mambo yakawa baam baaam. Dj Katambi akiwa nyuma ya mic na akaweka mabo sawa na kuwapoteza kabisaaa
 
Songa nasi kwa picha hapa.
 
Rangi: Red, Black na Gold



 

Thursday, December 5, 2013

Bi Khadija Kayumbu's Night at Leopard Hall

Akiwa na confidence za hatari, mrembo wa ukweli mwenye tabasamu la asili, Bi Khadija Kayumbu, aliingia kwa kujimwayamwaya ndani ya ukumbi mzuuuri wa kupendeza-Leopard Hall, D'salaam, akiwa na hamu ya kuwaonesha wageni waalikwa na marafiki na ndugu wa ukweli yuleee alokonga moyo wake...mumewe; Bw Hussein Isike!
 
Kwa nderemo na hoi hoi, ndugu wakafurahi na kujumuika nae kwa furaha. Wakicheza, wakiimba na kufurahi naye.
 
Kama kawaida, McNdimbo Crew na Respect Djs wakawasha moto wa hatareeee. Ilikua raha mustarehee; kuanzia Nigeria, South, Bongo Flava, mambo ya Pwani na cha kupendeza ni Gospoz za ukweli. Maids wakaweka ladha saaaafi; Sarah, Fetty, Happy na Scola
 
Songa nasi kwa picha.
 
Color: purple, yellow na red