Showing posts with label Kwalalumpa. Show all posts
Showing posts with label Kwalalumpa. Show all posts

Sunday, December 22, 2013

John Mabamba weds Pendo Alex @ Kwalalumpa, Sinza

Pale AIC, Chang'ombe, zikasikika kengele...ikiwa ni siku chache tu kabla ya Kristo kuzaliwa, Mtanashati John Shabani Mabamba akajongea kwa altare na kukutana na rafiki na neighbor wake wa ukweli, Bi Pendo Alex...kwa pamoja wakaapa kuishi pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha. Kiapo hicho kilifuatiwana nderemo na vifijo vya haja haswaaa
 
Wajita wale wakajichanganya na wakwe zao ambao ni wakurya...majirani asilia kutoka kule Mwilingo na Kiagata, Serengeti..wakafurahi kuunganisha undugu. Ni burudani ya haja kutoka kwa HB entertainment wakiwa na Respect Djs (Dj Bruno) na nyuma ya mic akawepo mdau wenu wa kawaida, McNdimbo!! Weee, taka tena kitu gani banaa. Ndani ya Kwalalumpa-Sinza hapo ni Cheza, ruka na jiachie ndo ukawa mpango mzima.
 
Kaka wa Bwana harusi, ambaye pia ni mlezi wake, Bw Moses Mabamba a.k.a Big Mo, akaonesha umahiri wa kulisakata sebene kwa kuweka chupa ya bia kwa kichwa na kujiachia apo akiwa na mpenzi mkewe Bi Witnes na wanao Dorry, Kurwa na Dotto.
 
Songa nasi kwa picha
 
Color Combo: Yellow, Red, Black na Gold
 
 
 
 
 
 

Monday, January 14, 2013

Don't Miss this... Gaspardus Gastus Mwombeki Weds Flavia GasparRutahindulwa @ Kwalalumpa, Sinza

Maneno mataaam ya wimbo mzuri wa Me & U wa Ommy Dimpoz yalirindima katika anga za ukumbi maarufu pale Sinza, Kwalalumpa, ambapo Bw Gaspardus akiingia na kipenzi chake Bi Flavia. Vifijo na nderemo viakasikika kutoka kila pannde za ukumbi huo. Marafiki zake na Gaspar wa enzi za useminarini kule Rubya Seminary, mashabiki wenzie wa soka wa ofisini wanajiita FORUM, wanaisimu na Lugha za kigeni kutoka UDSM na wengineo wakampa kampani ya kutosha.

Ndugu na Jamaa kutoka kuleee Bukoba vijijini na hasa vijiji vya Bwanja na Rukulungo wakaja na utamu wa kutosha wa Dereve Babili. Kwa kweli, maambo yalikua baam baaam! Dj Smol akiweka vitu adimu na mdau wa haja, The Blogger, nikawapa vionjo vya kidigitali vya 2013! Weeee... Burdaaaaani.

Kwa uchache, songa nasi kwa picha za matukio.

Color combo; Royal Blue na Pink Rose





















































Mr Taji na Mr Rutechura kwa mbaaaali


Mr Kelvin na wadau wa FLL wa UDSM


Mjasiriamali, Bw Asheri akiteta jambo


Wadau...


Maids













Jerusalem Vibrant Brothers...


Ze mkuki














Mkuu wa Idara ya FLL ya UDSM, Dr Upor akitoa neno kwa ufupi kwa ajili ya maharusi










Wazee wa FORUM wakiongozwa na Faraja Kristomus