Kazi nzuri na nyuma ya deck za muziki kukawa na mikono ya DjNdende. Hapa ilikua gospels tupu...hakuna uchakachuaji
Showing posts with label Wedding Planner. Show all posts
Showing posts with label Wedding Planner. Show all posts
Monday, May 11, 2015
Monday, March 30, 2015
MAANDALIZI YA HARUSI; KUCHAGUA SIKU YA HARUSI (Saving a Wedding Date)
Wadau wa blog yetu ya harusi,
Naamini tu wazima. Kuanzia sasa tutakua tunawaletea mfululizo wa habari za ujuzi wa maandalizi ya harusi. Hii inafuatia maombi ya wadau wengi baada ya kumsikiliza McNdimbo akidadavua mada mbalimbali kupitia kipindi cha Pongezi Maharusi Wetu kila Ijumaa kuanzia saa 10.00 jioni mpaka saa 11.00 hapo Morning Star Radio. Taarifa hizi zitakua zinakujia kila Jumatatu. Leo tutatoa VIDOKEZO vya Jinsi ya Kuchagua Siku ya Harusi

Umechumbiwa? Umechumbia? Hongera sana. Sasa swali linafuata ni harusi yenu lini? Sio rahisi sana kujibu hili ila mara nyingi ni vyema kuwa na muda wa kutosha kati ya uchumba hadi harusi ili kujipa nafasi ya kutosha kufanya maandalizi yenu vizuri. Ikiwezekana iwe hata mwaka mzima kabla.
1. KUMBUKUMBU
Siku mnayochagua kufunga ndoa inawakumbusha nini? Ni birthday ya mmoja wenu? Birthday ya mmoja wa wazazi wenu? ni wedding anniversary ya wazazi wenu? ni Siku ya Wapendanao? Muungano? Mothers' Day? Inapendeza kama ikiwa ni siku yenye kumbukumbu ya ziada.
2. NYAKATI ZA MWAKA (SEASON)
Ni vyema sana kua na picha na theme ya harusi yenu. Kama mnataka beach wedding kwa mfano, au mnataka kufanya shughuli hiyo katika ukumbi wa nje, itakua ngumu sana kuifanya nyakati za mvua. Mnapenda sherehe ya nyakati gani; mvua? Kiangazi? Joto au baridi?
3. GHARAMA
Je wajua bajeti inaweza kuathiri chaguzi lenu la siku ya kufanya sherehe ya harusi? Kuna nyakati ambazo vitu, ikiwemo mavazi hupanda sana. kwa mfano nyakati ziendazo na siku kuu kama Eid, Pasaka na Krismasi, gharama za vyakula na mavazi hupanda. Siku hizo sio muafaka za kufanya sherehe yenu kwa kuzingatia bajeti. Lakini pia kuna baadhi ya siku, kama Jumamosi, ambapo gharama za ukumbi na Ma-MC wazuri huwa na gharama za juu kuliko siku nyingine za wiki.
4. AINA ZA WAGENI
Kuna umuhimu pia kuangalia aina ya wageni wenu. Ni vyema kujua wale ndugu, jamaa na marafiki ambao mngependa wawepo katika siku yenu ya harusi. Saidianeni kupanga tarehe ya harusi yenu. Wafahamisheni alternatives mlizonazo. Itakua si jambo jema kupanga sherehe yenu katika siku ambayo watu wenu wa karibu watakua katika shughuli nyingine inayowalazimu kwenda; kwa mfano, anniversaries za ndoa zao, graduation au harusi za ndugu mwingine au mfanyakazi mwingine wa ofisini kwenu, birthdays n.k
Basi leo tuishie hapo na Jumatatu ijayo tutaendelea na Kipengele cha pili cha MAANDALIZI YA HARUSI...Jinsi ya Kutengeneza List ya wageni waalikwa ambayo ni determinant kubwa sana ya bajeti yenu ya harusi.
Lebo:
Harusi,
McNdimbo,
Send off,
Wedding Planner,
wedding planning
Monday, July 15, 2013
WHO IS MCNDIMBO!???
McNdimbo is a University Graduate holding a Master of Arts Degree in Linguistics, Professional Master of Ceremony,Events Planner, Motivational Speaker, Network Marketer, a Lecturer in language studies and Communication Skills and a Blogger.…
McNdimbo has worked as a language teacher in various secondary and high schools in Dar es Salaam. In the mean time he is a lecturer at Dar es salaam University College of Education (DUCE). He is an expert in planning and organizing events and weddings.He is a professional Master of Ceremony with experience of over ten years in planning, organizing and master the Weddings and Send off Parties,Corporate Events, Fund Rising and various Concerts .
McNdimbo is the Managing Director and a founder of McNdimbo Entertainment - a company dealing with Events and Wedding Planning and Management. He is the Blogger of www.ndimbomc.blogspot.com - a blog dedicated to wedding planning and associated events.
McNdimbo is dedicated to become the most vibrant,exciting,dynamic and successful Master of Ceremony, Motivational Speaker to enable the new generation building up their confidence and live their dreams.
Subscribe to:
Posts (Atom)



