Showing posts with label Picollo Hotels. Show all posts
Showing posts with label Picollo Hotels. Show all posts

Wednesday, September 18, 2013

William Kaposwe Weds Maria M'bade....Picolo Beach Hotel

Ukumbi ukiwa na nyuzi joto chache za kuwezesha waalikwa kujisikia kma wako nje ya jiji la Dar es Salaam, pembezoni mwa bahari ya Hindi... uwepo wa Mungu ukijidhihirisha na kuwapa faraja maharusi hao; Bw William Kaposwe na kipenzi chake Maria,wakafunga pingu za maisha pale Nayoth Church na kujimwaga hapo Grand Hall-Picolo Beach Hotel. Wakisindikizwa na marafki zao wa ukweli Bw Allen na mkewe Victoria, wana wa Mwandosya.

Kazi nzuri na burudani ya muziki ikidondoshwa na Respect Djs, chini ya utaalam wake Dj Pimbi ikawaweka katika kilele cha burudani wageni na familia zile. Kwa kuheshimu imani ya maharusi, familia na wageni wale, crew yetu ya burudani ikagawa full gospel style mwanzo mpaka mwisho wa sherehe ikwa na exceptions kidogo katika mtoko halisi wa kwaito.

Hakika burudani ilifika mahali pake...hii ndo raaaha ya McNdimbo Crew ktika kuhakikisha slogan yetu yafikiwa na kuboreshwa kila kukicha; YOUR SATISFACTION IS OUR PASSION!

Songa kwa picha hapa...

Colours: Aqua Green, Hot Pink na Baby Yellow

 


Friday, April 19, 2013

Picollo Hotels; Abraham Mcharo Mshana weds Clara Mabiki!!!!

Ilikua ni furaha ilioje, pale marafiki wawili wa siku nyingi, walipoamua rasmi kuvunja ukimya na sintofaham za siku kadha wa kadha ili kutimiza maandiko "...nae ataambatana na mkewe...". Abraham Mcharo Mshana kutoka Usangi kule Kilimanjaro na Bi Clara Mabiki wa mkoa mpya wa Njombe wakawa rasmi Mr & Mrs Abraham Mcharo Mshana. Hii ilifuatia kiapo maarufu "YES I DO" pale kanisa la KKKT, Kurasini. Shughli hiyo ikahamia pale Grande Hall, Picollo Hotels.

Wakiwa wamependeza na rangi zenye chaguzi kutoka mioyoni mwao, wakaingia kwa mbwembwe na tabasam la kutosha na huku wakicheka na kugonga mikono yao wakionesha ukaribu walio nao na haswaaaa, hapo ilikua ni destination yao. How sweeet!

Kampani ya kuyosha kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki ilikua ya haja haswaa. Their co-workers kutoka DUCE kwa Abraham na wale wa Minaki High school kwa Clara, hawakuwaacha wapweke. Wakacheza nao, serebuka kiukweli kwa uhondo kutoka kwa Dj Salim akisaidiwa uratibu na Mdau wenu hapa mwenye sauti adimu ya biashara. Kwa kweli, it was so great!!

Colours: silver na dark blue

Songa nasi...