Showing posts with label Lukolo. Show all posts
Showing posts with label Lukolo. Show all posts

Thursday, September 5, 2013

Lourine Jimmy's Fabulous Night...

Cha kwanza waweza kuona pale akitabasamu tu ni uleee mwanya...Mtoto wa Tanga huyo mwenye mwonekano wa kishombeshombe baab..LOURINE JIMMY. Ikafika wakati muafaka hapo ambapo aliamua ka moyo mkunjufu kuwaaga ndgu na jamaa ili akayaanze maisha ya ndoa takatifu na wake wa ukweli.
Wasambaa hao bila kushangaa wakajipanga vilivyo na kuamua kushirikisha ndugu, jamaa na marafiki ili kumuaga kipenzi wao katika ukumbi wa Lukolo, pale Tabata. Huku wakiwa na ucheshi wao wa asili na usongo wa haja wa kuburudika haswaaa na ngoma zao za asili bila ya kusahau maisha ya kiroho ya familia ile na kuburudika kwa nyimbo za injili na kumtukuza BWANA. Bila ajizi, crew nzima ya McNdimbo ikatoa ile raha ya ukweli na asili ya kukonga nyoyo za waalikwa. Hapo ni kata kiu mpaka kufikia malengo; YOUR SATISFACTION IS OUR PASSION....
 
Songa nasi kwa picha ...
 
Colours: Purple na Baby Yellow


Sunday, October 7, 2012

WHAT A PRE-WEDDING PARTY!! ANITA BISEKO @ LUKOLO SOCIAL HALL, D'SALAAM...SHUHUDIA

Akiwa amependeeza na tabasamu lake la asili na huku akionehsa umahiri wake wa kucheza muziki, aliingia na kuonesha designer wake na salooner walifanya kazi nzuri, ANITHA PALAPALA BISEKO alihitimisha shughuli yake ya kuagwa-Send off- pale katika ukumbi wa Lukolo, uliopo Tabata Jijini Dar es Salaam. Huku akiwa kasindindikizwa na mpambe wake, Bi Marysela Moshi, Bi Anitha alionekana mwenye furaha sana. Yote hiyo ni kwa kuwa ndoto zake za kuuacha ukapera na kuanza maisha yake mapya ya ndoa takatifu na wake wa ubani, Bw David Nkhungu zikionesha matumaini dhahiri. Utamu wa shughuli ulinogeshwa na wenyeji wa Ukerewe na kule kwa wakwe, Singida ambapo kulikua na wataalamu wa kucheza ile midundo ya asili ya huko. Tambaa nasi hapa ili uone yaliyojiri japo kwa uchache...

Color: Lemon Green & Pink

High Table

Mjikeki

Ukumbi Set Up

Bi Anitha (kushoto) na rafiki yake wakiingia kwa poz

Wakikaribishwa kwa burudani kama kawaida

Raaaaaaaha!

Kitu cha Maombi

Mwenyekiti Msaidizi, Mr Magoti akikaribisha rasmi wageni na kutambulisha wanakamati
Keki Tym

Kataaaa...kata!

Asanteni sanaaa
Kwa wazazi eee...
Muziki asili yake wapiiii...mziki ni burudiko la moyooo!
Thank you so very much..

Tuufurahiiii



Le Champaigne

Dushelele....

Jerusalem Vibrant Brothers nao walikuwapo

Anitha na David wake bnaaaa..

Mabestito.....