Showing posts with label Send off. Show all posts
Showing posts with label Send off. Show all posts

Wednesday, June 10, 2015

Monday, March 30, 2015

MAANDALIZI YA HARUSI; KUCHAGUA SIKU YA HARUSI (Saving a Wedding Date)

Wadau wa blog yetu ya harusi,




Naamini tu wazima. Kuanzia sasa tutakua tunawaletea mfululizo wa habari za ujuzi wa maandalizi ya harusi. Hii inafuatia maombi ya wadau wengi baada ya kumsikiliza McNdimbo akidadavua mada mbalimbali kupitia kipindi cha Pongezi Maharusi Wetu kila Ijumaa kuanzia saa 10.00 jioni mpaka saa 11.00 hapo Morning Star Radio. Taarifa hizi zitakua zinakujia kila Jumatatu. Leo tutatoa VIDOKEZO vya Jinsi ya Kuchagua Siku ya Harusi















Umechumbiwa? Umechumbia? Hongera sana. Sasa swali linafuata ni harusi yenu lini? Sio rahisi sana kujibu hili ila mara nyingi ni vyema kuwa na muda wa kutosha kati ya uchumba hadi harusi ili kujipa nafasi ya kutosha kufanya maandalizi yenu vizuri. Ikiwezekana iwe hata mwaka mzima kabla.





1. KUMBUKUMBU
Siku mnayochagua kufunga ndoa inawakumbusha nini? Ni birthday ya mmoja wenu? Birthday ya mmoja wa wazazi wenu? ni wedding anniversary ya wazazi wenu? ni Siku ya Wapendanao? Muungano? Mothers' Day? Inapendeza kama ikiwa ni siku yenye kumbukumbu ya ziada.

2. NYAKATI ZA MWAKA (SEASON)
Ni vyema sana kua na picha na theme ya harusi yenu. Kama mnataka beach wedding kwa mfano, au mnataka kufanya shughuli hiyo katika ukumbi wa nje, itakua ngumu sana kuifanya nyakati za mvua. Mnapenda sherehe ya nyakati gani; mvua? Kiangazi? Joto au baridi?

3. GHARAMA
Je wajua bajeti inaweza kuathiri chaguzi lenu la siku ya kufanya sherehe ya harusi? Kuna nyakati ambazo vitu, ikiwemo mavazi hupanda sana. kwa mfano nyakati ziendazo na siku kuu kama Eid, Pasaka na Krismasi, gharama za vyakula na mavazi hupanda. Siku hizo sio muafaka za kufanya sherehe yenu kwa kuzingatia bajeti. Lakini pia kuna baadhi ya siku, kama Jumamosi, ambapo gharama za ukumbi na Ma-MC wazuri huwa na gharama za juu kuliko siku nyingine za wiki.

4. AINA ZA WAGENI
Kuna umuhimu pia kuangalia aina ya wageni wenu. Ni vyema kujua wale ndugu, jamaa na marafiki ambao mngependa wawepo katika siku yenu ya harusi. Saidianeni kupanga tarehe ya harusi yenu. Wafahamisheni alternatives mlizonazo. Itakua si jambo jema kupanga sherehe yenu katika siku ambayo watu wenu wa karibu watakua katika shughuli nyingine inayowalazimu kwenda; kwa mfano, anniversaries za ndoa zao, graduation au harusi za ndugu mwingine au mfanyakazi mwingine wa ofisini kwenu, birthdays n.k

Basi leo tuishie hapo na Jumatatu ijayo tutaendelea na Kipengele cha pili cha MAANDALIZI YA HARUSI...Jinsi ya Kutengeneza List ya wageni waalikwa ambayo ni determinant kubwa sana ya bajeti yenu ya harusi.



Thursday, September 11, 2014

Dorothea a.k.a Dottie's Wonderful Night...at Diamond Jubilee

Sikuwahi kufikiria kwamba Diamond Jubilee ViP Hall ni ndogo!! Watu walifurika katika usiku mwanana wa Dorothea. Lakini sound nzito kutoka Respect Djs (shereheyetu.com)-Chini ya Dj Ndende, ikaunguruma na ikanakshiwa na sauti ya biashara ya mdau wenu hapa. ilikua hapatoshi....
 
songa nasi kwa picha nzuri kutoka kwa Shereheyetu Still na Video Productions - 0713324055


Saturday, July 5, 2014

AWESOME!!! MTOTO WA EAST AFRICA- AGNES HOPE HANTY @ MLIMANI CITY

Best Collaboration in town...kama kawaida; McNdimbo Entertainment na Respect Djs (www.shereheyetu.com)



Dj: Ndende
 
Rangi: Royal Blue,  Gold na Red
 
Songa nasi kwa picha






Wednesday, May 28, 2014

USIKU MWANANA WA BEATRICE

Kazi nzuri kutoka katika one of the best collaboration in the wedding industry; McNdimbo Entertainment na Respect Djs (www.shereheyetu.blogspot.com)
 
Ukumbi: Mwika Hall
 
Mc: Ndimbo

 
Dj: Ndende
 
Rangi: Purple na Baby Yellow
 
Songa nasi kwa picha
 


Friday, February 21, 2014

Thursday, January 23, 2014

EDA ASIMWE 2014 SPECIAL!! @ DUNKEEN HOUSE...

Akiwa na tabasamu la asili na kile mumewe mtarajiwa alichokiita "She looks Mmmmmmwaaaah", Bi Eda Asimwe, huku akisindikizwa na rafikiye mkyuut Irene, alijongea taratiiib ndani ya Ukumbi wa Dunkeen House, Mikocheni nakupokelewa kwa hamasa na nduguze wale kutoka Karagwena wengine wa nchi jirani.
Vijana wa HB Entertainmwnt wakatia chachandu katika chuzi la shughuli na kukoleza habari za kutoka Karagwe na kuweka uhalisia wa asili yake Bi Eda.
Bila ajizi wala shubiri, Mtanashati DJ Ndende, akawa nyuma ya mashine na kutoa budani isochosha kutoka Respect Djs (www.shereheyetu.blogspot.com) na kuwasha moto wa uhakika; kuanzia na kwaito, sebene, gospooz na mibongo ya fuleva ya kumwaga...achilia mbali zileeee za asili. Haposauti ilotulia ya mdau wenu ikiweka sawia utaratibu mzima wa shughuli ilopendeza haswaaa.
songa nasi kwa picha hapa
Colors: Pink na Silver