Tuesday, September 4, 2012

THIS WAS A WEDDING!! NOELI KWEKA TO AISAA SWAI...@ WERU WERU LODGE-MOSHI..

Nimefanya harusi nyingi sana, but THIS WAS A WEDDING!! Kwa kweli sikujuta kusafiri hadi Moshi kwa ajili ya ku-Mc this wedding! Iliandaliwa, ikaandalika. Wageni wakaalikwa na kualikika!! wee...Dar tumezoea kua na one-wing dish wedding...hapa nikakutana na two-wings dishes wedding. Mara baada ya harusi kufungwa katika kanisa la KKKT apo Moshi, tukasogea pembeni-Uhuru Hostel kwa ajili ya lunch. Lunch hii ilikua ni kwa heshima ya Baba Askofu Mstaafu Kweka ambaye pia ni baba mkubwa wa Bwana Harusi. Baada ya hapo msafara ukasonga mbele hadi WERU WERU LODGE, hoteli safi ya kitalii yenye mazingira mazuri sana...ndani ya garden ya maana...ambapo decor aliitengea haki haswaaa...pembeni kukiwa na Live Band ya Mark, chini ya uongozi wake Suleyman Pembe!! oh maammah!! Yaani ilikua burudaaaani...hapo takribani watu 800 na ushee wakawa mashuhuda wa harusi hii ya kihistoria kati ya Bw Noeli Samuel Kweka na Bi Aisaa Swai...

Color: Kachumbari; yellow, army green, gold, pink, red, white 

Theme: Nyama Choma mixed! utaitaka!

Tiririka nasi hapa kidooogo

Bw Noeli Kweka na mkewe Bi Aisaa Noeli Kweka, mara baada ya kufunga pingu za maisha.

Wakiwa na tabasaaam

Maids wakiwa wanashuulika na zawadi...

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akiteta jambo na maharusi

Mara baada ya lunch hapo Uhuru Hostel, maharusi wakijiandaa kuondoka

Nikakapenda kagari ka maharusi aseee!!


Miji-Vogue kwa ajili ya wazazi

Decor!! Ze kachumbariii

What a place!! A swimming pool pembeni...

Msafara huoooo...

Kitu 'mando' kwa ajili ya mapaparazzi


Hapa ni eneo la kuota moto!!

Seat Plan! colours zooote...hakuna kisingizio cha oooh! Mie sina gauni la rangi ya harusi!

Watoto Hawaruhusiwi?? Sawaa, ila wale watoto ving'ang'anizi Je?? Wapige na jumping Castles zao apoo

Mji-cake sasa huooooo...

Kwa heshima ya maharusi...na tusimame

Burudani banaaa

Mdau akiongoza wataalamu wa KWAITOOOz

Mdau akiwa na The Mark Band; nayo ilitoka Dsm...Hawa jamaa ni noumar!! Wanapiga charanga, rhumba, reggae, mduara, za dini na ragga!! Hakuna kitu haipo apo..

Maharusi wakifuraaaahi....mabest friends hao

Maids na poz lao..ndani ya army green..

Mr na Dr KimiNA wakiwa ndo wasindikizaji wa maharusi apo..

Bw na Bi Kweka (kushoto); Wazazi wa Bw Harusi

Bw Robert; Mkurugenzi wa Omni Studio, akipata picha za kumbukumbu apo

Burudani kwa kwenda mbele; ndo mpango mzima

Unataka ubwabwa?? Kale kwenu uko...apo ilikua ni nyama choma tu; kuku, mbuzi na ng'ombe tu...kula na kunywa hadi majogoo

Tule sisi


1 comment:

GaraB said...

Ebwanae hii Wed ilikua BaaBkubwa,and am sure umeitendea haki maana imekusafirisha toka Dsm.U GaraBig Up za kutosha toka kwangu broda Ndimbo da Mc!