Thursday, April 23, 2015

USIKU WA VERONICA RICHARD MAEMBE AT KRISTO MFALME

Kazi nzuri ya iliyosimamiwa nasi kwa kushirikiana na Respect Djs chini ya kijana mtanashati, DjNdende
 
songa nasi kwa picha
 
 

Wednesday, April 8, 2015

MAANDALIZIYA HARUSI; JINSI YA KUTENGENEZA ORODHA YA WAGENI WAALIKWA

Leo wadau wetu wa harusi tutajikita katika jinsi gani unaweza kutengeneza orodga ya wageni waalikwa (wedding guests list)

Kimsingi, ni ngumu sana kuandaa sherehe bila kujua idadi ya watu unaowaalika. Hii ndio huweza kukupa uwezo wa kufanya maamuzi ya bajeti nzima. Bila kujua idadi ya waalikwa basi hata kuweza kuamua ukumbi wa sherehe inakua ngumu,. Nimekutana na wateja mara kadhaa ambao wanataka kuandaa sherehe na huku wanadai wana watu kama mia tu ila mwisho wa siku anakuta ana watu 700!! Hapo inaweza kukuletea shida sana katika kufanya maamuzi ya bajeti. Fanya kufahamu idadi ya wageni waalikwa watarajiwa, tena kwa majina yao. Hii ifanyiketakribani miezi 10 au mwaka mzima kabla. Waweza kua unaihariri siku zinavyosonga.


Wawezaje kutengeneza list hii

1. Orodha ya Kitabu cha simu (Phone book)
 
Ni rahisi sana kujua ni nani mwaweza kumualika kwa kutumia orodha ya wale walioko katika simu zenu. Humo kuna watu wenu wa karibu sana na ambao mnawasiliana mara nyingi. Hapo wapo ndugu, jamaa na marafiki. Waandike katika orodha uliyoiandaa.

2. Tumieni Ndugu zenu
 
Ni vizuri kuwashirikisha ndugu zenu katika kuandaa orodha hii. Mathalani wazazi wenu; hawa lazima watakua na ndugu, jamaa na marafiki zao wanaoamini watakuja kwa shughuli yenu. Kaka na dada zenu pia watakua namarafiki watakaopenda kuwaalika. Na kadhalika

3. Wafanyakazi wenzenu na majirani
 
Hawa ni wa kuwapa kampani ya ukweli. Kuna harusi nilizofanya zimebebwa sana na marafiki wafanyakazi. Wakuta mtu wazazi wanaishi mkoani ila wafanyakazi wenzao na majirani wanakua wamechangamsha sherehe na ndio washika dau wakubwa.

4. Vikundi vya kijamii
 
Hii hushirikisha wale mnaokua nao pamoja katika mambo mengi ya kijamii; Wale mnaosali nao pamoja, mpo nao kwa vilabu vya mazoezi na michezo, siku hizi kuna groups za WhatsAPP na Facebook na wengine.
 
Kwa ujumla wake, unaalika watu ambao k namna moja au nyingine mnnaweza kujisikia furaha na ku have enough fun wanapoka pamoja nanyi.
 
Asanteni..tukutane tena wakati ujaotuangalie Jinsi ya Kutafuta Ukumbi wa sherehe

Friday, April 3, 2015

We wish a Wonderful Easter

Crew nzima ya McNdimbo Entertainment na  Respect Djz, tungependa kuwatakia Heri ya Pasaka wateja wetu.
Tunaamini itakua ni wakati mzuri na wenye furaha kwetu.
Tunaahidi kuendelea kuwapa burudani thabiti na wakati mzuri katika kazi mlizotuamini nazo mara tu baada ya Pasaka.

Asanteni.

Monday, March 30, 2015

MAANDALIZI YA HARUSI; KUCHAGUA SIKU YA HARUSI (Saving a Wedding Date)

Wadau wa blog yetu ya harusi,
Naamini tu wazima. Kuanzia sasa tutakua tunawaletea mfululizo wa habari za ujuzi wa maandalizi ya harusi. Hii inafuatia maombi ya wadau wengi baada ya kumsikiliza McNdimbo akidadavua mada mbalimbali kupitia kipindi cha Pongezi Maharusi Wetu kila Ijumaa kuanzia saa 10.00 jioni mpaka saa 11.00 hapo Morning Star Radio. Taarifa hizi zitakua zinakujia kila Jumatatu. Leo tutatoa VIDOKEZO vya Jinsi ya Kuchagua Siku ya HarusiUmechumbiwa? Umechumbia? Hongera sana. Sasa swali linafuata ni harusi yenu lini? Sio rahisi sana kujibu hili ila mara nyingi ni vyema kuwa na muda wa kutosha kati ya uchumba hadi harusi ili kujipa nafasi ya kutosha kufanya maandalizi yenu vizuri. Ikiwezekana iwe hata mwaka mzima kabla.

1. KUMBUKUMBU
Siku mnayochagua kufunga ndoa inawakumbusha nini? Ni birthday ya mmoja wenu? Birthday ya mmoja wa wazazi wenu? ni wedding anniversary ya wazazi wenu? ni Siku ya Wapendanao? Muungano? Mothers' Day? Inapendeza kama ikiwa ni siku yenye kumbukumbu ya ziada.

2. NYAKATI ZA MWAKA (SEASON)
Ni vyema sana kua na picha na theme ya harusi yenu. Kama mnataka beach wedding kwa mfano, au mnataka kufanya shughuli hiyo katika ukumbi wa nje, itakua ngumu sana kuifanya nyakati za mvua. Mnapenda sherehe ya nyakati gani; mvua? Kiangazi? Joto au baridi?

3. GHARAMA
Je wajua bajeti inaweza kuathiri chaguzi lenu la siku ya kufanya sherehe ya harusi? Kuna nyakati ambazo vitu, ikiwemo mavazi hupanda sana. kwa mfano nyakati ziendazo na siku kuu kama Eid, Pasaka na Krismasi, gharama za vyakula na mavazi hupanda. Siku hizo sio muafaka za kufanya sherehe yenu kwa kuzingatia bajeti. Lakini pia kuna baadhi ya siku, kama Jumamosi, ambapo gharama za ukumbi na Ma-MC wazuri huwa na gharama za juu kuliko siku nyingine za wiki.

4. AINA ZA WAGENI
Kuna umuhimu pia kuangalia aina ya wageni wenu. Ni vyema kujua wale ndugu, jamaa na marafiki ambao mngependa wawepo katika siku yenu ya harusi. Saidianeni kupanga tarehe ya harusi yenu. Wafahamisheni alternatives mlizonazo. Itakua si jambo jema kupanga sherehe yenu katika siku ambayo watu wenu wa karibu watakua katika shughuli nyingine inayowalazimu kwenda; kwa mfano, anniversaries za ndoa zao, graduation au harusi za ndugu mwingine au mfanyakazi mwingine wa ofisini kwenu, birthdays n.k

Basi leo tuishie hapo na Jumatatu ijayo tutaendelea na Kipengele cha pili cha MAANDALIZI YA HARUSI...Jinsi ya Kutengeneza List ya wageni waalikwa ambayo ni determinant kubwa sana ya bajeti yenu ya harusi.Thursday, March 26, 2015

Msimu Unaanza

Baada ya mapumziko ya wiki kadhaa za Kwaresima, crew nzima ya McNdimbo na Respect Djs soon inarudi na kuendeleza uhondo wa burudani.

Kwa sasa tunakuja na product mpya katika package nzima ya sherehe ambapo tutakupa stickers katika champein zako zote ukumbini. Stickers hizi ni bure kabisa. Zitakua na picha ya maharusi na zaidi zikiwa na kumbukumbu ya ukumbi, tarehe na maneno ya shukurani.

Tuamini. Tukushangaze