Sunday, June 24, 2012

MASTER OF CEREMONY; NDO SHEREHE YENYEWE?

Kuna wakati ninaalikwa katika sherehe, yaani mie nakua back bencher, huwa nakua na hamu saana ya kumuona mtendaji kazi mwenzangu (Mc) anavyoipeleka sherehe. sio siri, kuna challenges sana ya uendeshaji wa sherehe. Ukiwa Mc hauzioni ila unaziona vizuri sana ukimuona mwenzio anaendesha shughuli fulani. Kuna wakati nafurahi sana na kuamini kuna watu wamebarikiwa kuwa maMC ila kuna wakati naboreka ile mbayaaaa. Huwa najiuliza, huyu kapewa hii kazi kwa kujitolea au ni ndugu wa wenye shughuli na wamempa kazi hii ajifunze. Worse enough waweza kukutana na the same person katika kazi nyingine na akawa katika kiwango kile kile cha awali.

Mc Natalis Natalis


Nimeendesha shughuli za maofisini kidogo; za kumaliza na kukaribisha mwaka, za kutoa zawadi na kupongezana, za kuwaaga mabosi nk.Lakini nimeendesha shughuli nyingi zaidi za harusi; weddings, send off parties etc. Kuna mambo ya msingi sana nimejifunza Mc hana budi kuwa na ufahamu kabla ya kuendesha shughuli yoyote ile.
Mc Foma Foma

Kwanza kabisa ni aina ya shughuli yenyewe; harusi? send off? cooperate event? tamasha? or what? ni muhimu saaa kujua audience yako; Vijana, wazee, mchanganyiko?

Kama ni harusi, ni ya utamaduni gani (makabila), ni ya kiislamu au kikristo? hakuna kitu kinaboa kama kumkuta Mc anazungumzia champein wakati wahusika wala hawaitaki kabisaaa, kutokana na maadili yao ya dini. Au unafanya harusi ya wahaya halafu unawaita wazazi waende wakapeleke zawadi kwa maharusi!! Ni muhimu sana kujua mila za wahusika na imani zao za dini na kuziheshimu.

Mc Adelly Ngaya
Ukiwa mjuvi wa aina ya watu unaofanya nao shughuli, itakuwia rahisi sana Mc na Dj kujua aina ya muziki ambao audience yako inaweza ku-enjy.

Mc Luvanda Anthony
Zaidi, ni muhimu sana kwa Mc kujali muda. Hakuna raha kufanya sherehe na watu wanajikuta wanapata dinner saa 5 au 6 usiku!! Chagua ratiba nzuri, kuna wakati utalazimika kubadilisha ratiba yako ili kuwafanya watu waenjy sherehe lakini pia wapate chakula katika wakati ambao ni most convenient. Kuna siku nililzimika kumuingiza bibi arusi, katika send off kwa mbwembwe na alipofika mbele, tukapiga sala na kwenda kula kabisaaaa!! wakwe wamekuja saa 3.40 usiku na ukumbi unazima taa saa 6 usiku, apo inakuwaje??



Wanakamati wana challenges sana za kujua uzoefu wa maMC. kuna wakati unakuta umependekezwa kwenye kamati, anakujua mtu mmoja tu na tena hana influence kwa kwa kamati. Hata hivyo, ukiwakuta wanakamati makini, wakifanya interview nzuri, hawasiti kujua ni nani anastahili kufanya kazi yenye hadhi ya kamati yao.
Mc Double A akiwa na Mh Rais Jakaya Kikwete

Ushauri wangu kwa watendaji wenzangu ni kwamba, ukipata kazi ya watu basi ifanye kwa nguvu na akili zako zote ili kuendelea kujenga jina zuri la watendaji hapa nchini. Kama wajua haupo na nafasi uwe mkweli ili io kazi apewe mtendaji mwenzio na sio unategemewa wewe halafu unawapelekea Mc mwingine bila hata ya kuwataarifu. Hata kama uyo Mc mwiegine ni mzuri saaana, bado imani yako kwa wanakamati inakua ndogo na unawafanya waamini kwamba maMc wote wana tabia hiyo.

Cover Photo
McNdimbo


SAA DAIMA; HUDUMA BORA

No comments: