Wednesday, September 25, 2013

Filbert Kinunda Weds Cellina Muhe...... @ Mbezi Garden Hotels

Raha ya wamatengo, wacheze n kufuraahi...basi hapo tabasamu kwa sura na mioyo yao halikauki. Hapa ilikua siku maalum kabisa kwa Bw Filbert Kinunda kutoka kuleee Mbinga na Bi Celina Muhe mwenye asili ya Wairaki kutoka mkoa wa Arusha. Hawakua na sababu ya kutoamini yale yalioandikwa...wakawaacha baba na mama zao, wakajongea madhabahu ya Kanisa la Elshaddai Temple International na kuambatana rasmi wakiwa Mr & Mrs Filbert Kinunda. Maharusi hao walisindikizwa na marafiki zao wa siku nyingi; Bw na Bi Davis Nyanda.
 Burudani safi kutoka kwa Kwayu Music Classic chini ya Dj Danny na uhondo wa Mdau hapa, shughuli safi ile ndani ya ukumbi murua wa Mbezi Garden Hotels ikageuka ni ukumbi wa burudani na huku tukipata maneno ya busara kutoka kwa Mchungaji Kinunda na wakwe.
Songesha hapa kwa uhondo zaidi
Colours; Baby yellow, black na purpleNo comments: