Sunday, December 22, 2013

John Mabamba weds Pendo Alex @ Kwalalumpa, Sinza

Pale AIC, Chang'ombe, zikasikika kengele...ikiwa ni siku chache tu kabla ya Kristo kuzaliwa, Mtanashati John Shabani Mabamba akajongea kwa altare na kukutana na rafiki na neighbor wake wa ukweli, Bi Pendo Alex...kwa pamoja wakaapa kuishi pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha. Kiapo hicho kilifuatiwana nderemo na vifijo vya haja haswaaa
 
Wajita wale wakajichanganya na wakwe zao ambao ni wakurya...majirani asilia kutoka kule Mwilingo na Kiagata, Serengeti..wakafurahi kuunganisha undugu. Ni burudani ya haja kutoka kwa HB entertainment wakiwa na Respect Djs (Dj Bruno) na nyuma ya mic akawepo mdau wenu wa kawaida, McNdimbo!! Weee, taka tena kitu gani banaa. Ndani ya Kwalalumpa-Sinza hapo ni Cheza, ruka na jiachie ndo ukawa mpango mzima.
 
Kaka wa Bwana harusi, ambaye pia ni mlezi wake, Bw Moses Mabamba a.k.a Big Mo, akaonesha umahiri wa kulisakata sebene kwa kuweka chupa ya bia kwa kichwa na kujiachia apo akiwa na mpenzi mkewe Bi Witnes na wanao Dorry, Kurwa na Dotto.
 
Songa nasi kwa picha
 
Color Combo: Yellow, Red, Black na Gold
 
 
 
 
 
 





























 


























 

















 





































No comments: