Sunday, December 15, 2013

ELICE MREMA is sent off at KRISTO MFALME in Dar es Salaam...

Akiwa na kumbukumbu za nyumbani, Tanzania, baada ya kuondoka kwa muda wa zaidi ya miaka saba na kwenda kuishi Marekani, Elice Mrema, akarudi na kuja kuagwa rasmi ili apate Baraka za kuolewa na kuishi na kipenzi na rafiki yake wa ukweli, Francis Thairu.
 
Shughuli hiyo ikiwa na muonekano wa kimataifa zaidi, ambapo bwana harusi ana asili ya County ya Kiambuu kwa kijiji cha Kabete karibu kabisa na Nairobi. Huu ni muungano wa haja wa Afrika ya Mashariki.
 
Furaha na nderemo zikasikika hapo ndani ya ukumbi wa Kristo Mfalme hapo Tabata, jiji la Dar es Salaam. Wachagga wakashikana mikono na wakikuyu wakijiachia kwa furaha kabisaa.
 
Crew nzima ya McNdimbo kwa kushirikiana na Respect Djs (www.shereheyetu.blogspot.com) wakawasha moto. Zikapigwa za Kenya na za Tz na mambo yakawa baam baaam. Dj Katambi akiwa nyuma ya mic na akaweka mabo sawa na kuwapoteza kabisaaa
 
Songa nasi kwa picha hapa.
 
Rangi: Red, Black na Gold



 



















 


























 








































 
 
 
 

No comments: