Wednesday, April 8, 2015

MAANDALIZIYA HARUSI; JINSI YA KUTENGENEZA ORODHA YA WAGENI WAALIKWA

Leo wadau wetu wa harusi tutajikita katika jinsi gani unaweza kutengeneza orodga ya wageni waalikwa (wedding guests list)

Kimsingi, ni ngumu sana kuandaa sherehe bila kujua idadi ya watu unaowaalika. Hii ndio huweza kukupa uwezo wa kufanya maamuzi ya bajeti nzima. Bila kujua idadi ya waalikwa basi hata kuweza kuamua ukumbi wa sherehe inakua ngumu,. Nimekutana na wateja mara kadhaa ambao wanataka kuandaa sherehe na huku wanadai wana watu kama mia tu ila mwisho wa siku anakuta ana watu 700!! Hapo inaweza kukuletea shida sana katika kufanya maamuzi ya bajeti. Fanya kufahamu idadi ya wageni waalikwa watarajiwa, tena kwa majina yao. Hii ifanyiketakribani miezi 10 au mwaka mzima kabla. Waweza kua unaihariri siku zinavyosonga.


Wawezaje kutengeneza list hii

1. Orodha ya Kitabu cha simu (Phone book)
 
Ni rahisi sana kujua ni nani mwaweza kumualika kwa kutumia orodha ya wale walioko katika simu zenu. Humo kuna watu wenu wa karibu sana na ambao mnawasiliana mara nyingi. Hapo wapo ndugu, jamaa na marafiki. Waandike katika orodha uliyoiandaa.

2. Tumieni Ndugu zenu
 
Ni vizuri kuwashirikisha ndugu zenu katika kuandaa orodha hii. Mathalani wazazi wenu; hawa lazima watakua na ndugu, jamaa na marafiki zao wanaoamini watakuja kwa shughuli yenu. Kaka na dada zenu pia watakua namarafiki watakaopenda kuwaalika. Na kadhalika

3. Wafanyakazi wenzenu na majirani
 
Hawa ni wa kuwapa kampani ya ukweli. Kuna harusi nilizofanya zimebebwa sana na marafiki wafanyakazi. Wakuta mtu wazazi wanaishi mkoani ila wafanyakazi wenzao na majirani wanakua wamechangamsha sherehe na ndio washika dau wakubwa.

4. Vikundi vya kijamii
 
Hii hushirikisha wale mnaokua nao pamoja katika mambo mengi ya kijamii; Wale mnaosali nao pamoja, mpo nao kwa vilabu vya mazoezi na michezo, siku hizi kuna groups za WhatsAPP na Facebook na wengine.
 
Kwa ujumla wake, unaalika watu ambao k namna moja au nyingine mnnaweza kujisikia furaha na ku have enough fun wanapoka pamoja nanyi.
 
Asanteni..tukutane tena wakati ujaotuangalie Jinsi ya Kutafuta Ukumbi wa sherehe

No comments: