Tuesday, May 29, 2012

RAHA YA SHEREHE YA HARUSI

McNdimbo 'Mwana Wa Mshike Mshike' akisherehesha uko Arusha
Watu wengi wamekua na mkanganyiko wa kufahamu ni kwa jinsi gani waweza kuwa na harusi yenye mvuto. akuna watendaji wengi sana katika nyanja za sherehe na harusi hapa Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla. Yawezekana ukaona ni rahisi sana kuwa na sherehe nzuri na ya kupendeza kwa kua tu umekusanya au una hela ya kukutosha sana kwa ajili ya harusi yako. Kuna harusi zina bajeti ya Tshs Milioni 30 na hata zaidi. Nyingine zina bajeti ya Milioni 5 au chini ya hapo. Ni rahisi sana kufikiri kwamba harusi ya Mil 30 itafana kuliko ile ya Mil5. Ila ukweli ni kwamba harusi ni kuipangilia kwa uangalifu mkubwa. Kujiepusha saaaana na wajumbe wa kamati matapeli. Wajumbe wanaotaka 10% kutoka kwa watendaji dhaifu na wasio waaminifu katika kazi. Wajumbe wa aina hii, watakuletea wapishi dhaifu, wapambaji dhaifu, wapiga picha wasiojua wajibu wao na wakati mwingine (worse enough) watakuletea MC wa ajabu, anayejua kusoma ratiba tu. Sherehe ikawa so dull na watu wakaishia kulewa na kuangalia shughuli ikiwa ni vituko vitupu!!

Matarajio yangu ni kwamba, blog hii itatoa mwangaza wa kutosha kukuonesha ni kwa kiasi gani unaweza kutuamini McNDIMBO ENTERTAINMENT kukuwezesha kufanya sherehe nzuri na ya kiwango cha juu kabisa. Hii ni kwa kukuwezesha kufanya kazi na watendaji waliobobea na wanaojua majukumu yao. LET US PLAN YOUR WEDDING! kwa gharama nafuu na hutajuta kabisaaa.

K A R I B U N A T U W E P A M O J A ! !

No comments: