Tuesday, December 31, 2013

Maurice Njowoka weds Paulina Msanga @ Sunset-Tembo; Diamond Atumbuiza!!

Wamanda na Wapare!! Yaani hapo shughuli lazima ibambe....mwendo mdundo!! Tuserebukeee aeee aeeee....mara huku...libegho la mwana li hajaaa...aeeee lihajaaa! weee
Maurice Njowoka, Meneja wa Coca Cola Light, akiwa na tabasamu lake asilia akasahau mambo yake ya marketing kwa muda na kumuangalia usoni mtoto wa kipare, mrembo wa asili, Bi Paulina Msanga na kumvisha pete ya dhahabu kidoleni, huku akitamka maneno yatarajiwayo "For bera for worse..." paleeeee RC-Sinza na kutamkwa rasmi kuwa
Mr & Mrs Maurice Edwin Njowoka.
Vigelegele na nderemo za haja vikaanza hapo , huku wamanda wakigalagala chini kuonesha kupendezwa na kukubalika kwa tukio lile la kihistoria. Hapo nje kanisani watu wakacheza Lindeku (ngoma ya watu wa Manda, Songea) na kujiachia haswaaaa.
Shughuli ikahamia paleee Mbezi Beach katika ukumbi maarufu wa Sunset-Tembo Hall. Kumbi likasheheni na kutapika watu takribani 700!! Hapo nyuma ya mashine yupo Dj Ndende kutoka Respect Djs (www.shereheyetu.blogspot.com) na katikati nipo mdau na blogger wenu. Tukawasha moto wa hatareeee. Hiyo ni trelaaa...ikaja ngoma ya mganda na baadaye Jerry Mtumishi akatoa burudani yake.
Ikaja surprise ya kufungia mwaka sasa...kwa mbaaali ikasikika sauti yake "tatizo kwetu mbagalaaaaa..", akaongeza tena '..you are my number one..my swt.." hahahahahaa! Kitu cha Diamond Platnumzzzz!! Watu wakapagawaaaa...yaani ni burudani kwa kwenda mbele!! What else did we have to say? Hii ilikua harusi iliyostahili kufunga mwaka kwa crew nzima ya McNdimbo Entertainment!!
YOUR SATISFACTION IS OUR PASSION
Songa nasi kwa picha
Colours: Aqua Green, Silver na Red













































































No comments: