Saturday, January 4, 2014

Nkunzi 2014 Special At Kiramuu Hall

Nderemo na vifijo vilisikika kwa haja pale ndani ya ukumbi wa ukweli: KIRAMUU Hall, Mbezi Beach Dar es Salaam, pale ambapo mtoto wa kiha, binti wa zamani wa PCM pale Kilakala, Eng. Nkunzi James Nyabakari alipokua akiingia kwa tabasamu la haja!! Huku akisindikizwa na rafiki yake kipenzi, Lyidya kwa pembeni, Engineer Nkunzi wa Tanrod akatembea kwa maringo na urefu wake mithili ya twiga, akanyanyua mkono juu kwa madaha na kuwasalimia ndugu, jamaa na marafiki waliojazana kushuhudia kuagwa kwake. Raaaaha Mustarehe.

Ngugu zaqke, waha wale wakapagawishwa na uhondo wa nyimbo za kwao "...indegeee inooobhobhaaa...." na vionjo vya Upendo Nkone katika lugha yake ya asili. Dj Ndende kutoka Respect Djs, akawapoteza na wakapotea kabisaa.
Kampani yake ya PCM-Kilakala; Neema Kisha, Reme, Hekima, Irene Lucian, Dorothy, Ney Opiyo, Rita, Rose na Rachel wakawa nae kwa karibu wakimshangilia Engineer mwenzao huyo.
Mabest wengine, Watanashati wa Mujiiiini, wakiongozwa na Madam Chairperson; Leyla Bhanji na Admini Adel(McDouble A) ambaye alikua pia mshenga, Lizzy, Joanita, Jamila kutoka Kilombero na Mdau McNdimbo...wakalifanya tabasamu la Nkunzi lisikauke kabisaa mpaka usiku mkubwa shughuli ilipogota kwa ukingo. Ilikua ni shidaaaaah!!

Songa nasi kwa picha
Colors: Aqua Green, hot pink na Silver 
No comments: