Thursday, January 23, 2014

EDA ASIMWE 2014 SPECIAL!! @ DUNKEEN HOUSE...

Akiwa na tabasamu la asili na kile mumewe mtarajiwa alichokiita "She looks Mmmmmmwaaaah", Bi Eda Asimwe, huku akisindikizwa na rafikiye mkyuut Irene, alijongea taratiiib ndani ya Ukumbi wa Dunkeen House, Mikocheni nakupokelewa kwa hamasa na nduguze wale kutoka Karagwena wengine wa nchi jirani.
Vijana wa HB Entertainmwnt wakatia chachandu katika chuzi la shughuli na kukoleza habari za kutoka Karagwe na kuweka uhalisia wa asili yake Bi Eda.
Bila ajizi wala shubiri, Mtanashati DJ Ndende, akawa nyuma ya mashine na kutoa budani isochosha kutoka Respect Djs (www.shereheyetu.blogspot.com) na kuwasha moto wa uhakika; kuanzia na kwaito, sebene, gospooz na mibongo ya fuleva ya kumwaga...achilia mbali zileeee za asili. Haposauti ilotulia ya mdau wenu ikiweka sawia utaratibu mzima wa shughuli ilopendeza haswaaa.
songa nasi kwa picha hapa
Colors: Pink na SilverNo comments: