Monday, April 29, 2013

Deluxe, Sinza; Ukende Masangya is Sent Off!!! What a Day!

Huku kiyoyozi kikiwa kimesetiwa kwa nyuzi 22 za centigrade, Bi harusi Mtarajiwa Ukende Elia Masangya na best yake Brenda wakaingia kwa raha zao. Nderemo na vifijo kutoka kwa wanyiramba wale zikarindima pale katika ukumbi maarufu jiji la Dar es Salaam, Deluxe Sinza Kwa Wajanja.

Akiwa kavalia gauni lililomkaa vyema na rangi safi aloichagua mwenyewe. Kitu cha peach! Mashostito na marafiki wa ukweli kutoka Airtel- anakofanyia kazi, mabest wa UDSM anakosoma Mastaz ya Biashara za Kimataifa, ndugu, jamaa na marafiki wakaungana naye katika usiku wake Bi ukende na kufurahi.

Mdau, kama kawaida hapo, nikisaidiana na Dj makini kabisa, Dj Smol, tukawarusha kwa mikwaito ya kuanzia...uo ukawa ndo uzinduzi. Wanyiramba wakaramba ile "zigiziiii, zigiziii....songelaaaa" kutoka kwa Rose Mhando... Wale wakwe zake, wahehe kutoka kule Iringa wakaduwa na nyimbo za kwao na baadaye tukamalizia na mixture ya hataaari ikiwa na zile za zamani, za west Afrika, za taarabu na zile za DRC! Ilikua ni mshikemshike kuleta ukweli wa "Your Satisfaction is our Achievement"

Songa nasi apa kwa picha...

Colours; Peach, Lavender na Hot Pink

 

No comments: