Monday, March 30, 2015

MAANDALIZI YA HARUSI; KUCHAGUA SIKU YA HARUSI (Saving a Wedding Date)

Wadau wa blog yetu ya harusi,
Naamini tu wazima. Kuanzia sasa tutakua tunawaletea mfululizo wa habari za ujuzi wa maandalizi ya harusi. Hii inafuatia maombi ya wadau wengi baada ya kumsikiliza McNdimbo akidadavua mada mbalimbali kupitia kipindi cha Pongezi Maharusi Wetu kila Ijumaa kuanzia saa 10.00 jioni mpaka saa 11.00 hapo Morning Star Radio. Taarifa hizi zitakua zinakujia kila Jumatatu. Leo tutatoa VIDOKEZO vya Jinsi ya Kuchagua Siku ya HarusiUmechumbiwa? Umechumbia? Hongera sana. Sasa swali linafuata ni harusi yenu lini? Sio rahisi sana kujibu hili ila mara nyingi ni vyema kuwa na muda wa kutosha kati ya uchumba hadi harusi ili kujipa nafasi ya kutosha kufanya maandalizi yenu vizuri. Ikiwezekana iwe hata mwaka mzima kabla.

1. KUMBUKUMBU
Siku mnayochagua kufunga ndoa inawakumbusha nini? Ni birthday ya mmoja wenu? Birthday ya mmoja wa wazazi wenu? ni wedding anniversary ya wazazi wenu? ni Siku ya Wapendanao? Muungano? Mothers' Day? Inapendeza kama ikiwa ni siku yenye kumbukumbu ya ziada.

2. NYAKATI ZA MWAKA (SEASON)
Ni vyema sana kua na picha na theme ya harusi yenu. Kama mnataka beach wedding kwa mfano, au mnataka kufanya shughuli hiyo katika ukumbi wa nje, itakua ngumu sana kuifanya nyakati za mvua. Mnapenda sherehe ya nyakati gani; mvua? Kiangazi? Joto au baridi?

3. GHARAMA
Je wajua bajeti inaweza kuathiri chaguzi lenu la siku ya kufanya sherehe ya harusi? Kuna nyakati ambazo vitu, ikiwemo mavazi hupanda sana. kwa mfano nyakati ziendazo na siku kuu kama Eid, Pasaka na Krismasi, gharama za vyakula na mavazi hupanda. Siku hizo sio muafaka za kufanya sherehe yenu kwa kuzingatia bajeti. Lakini pia kuna baadhi ya siku, kama Jumamosi, ambapo gharama za ukumbi na Ma-MC wazuri huwa na gharama za juu kuliko siku nyingine za wiki.

4. AINA ZA WAGENI
Kuna umuhimu pia kuangalia aina ya wageni wenu. Ni vyema kujua wale ndugu, jamaa na marafiki ambao mngependa wawepo katika siku yenu ya harusi. Saidianeni kupanga tarehe ya harusi yenu. Wafahamisheni alternatives mlizonazo. Itakua si jambo jema kupanga sherehe yenu katika siku ambayo watu wenu wa karibu watakua katika shughuli nyingine inayowalazimu kwenda; kwa mfano, anniversaries za ndoa zao, graduation au harusi za ndugu mwingine au mfanyakazi mwingine wa ofisini kwenu, birthdays n.k

Basi leo tuishie hapo na Jumatatu ijayo tutaendelea na Kipengele cha pili cha MAANDALIZI YA HARUSI...Jinsi ya Kutengeneza List ya wageni waalikwa ambayo ni determinant kubwa sana ya bajeti yenu ya harusi.No comments: