Tuesday, August 27, 2013

What a Wedding! Davis Nyanda weds Martha Kisandu

Furaha na nderemo za kutosha kutoka kwa wasukuma wa pande mbili; The Nyandas na The Kisandus zilisikika kila pembe kufuatia kijana mtanashati, mpole na mwenye uzelendo wa kisukuma hasaaa, Davis Nyanda alipofunga pingu za maisha na kipenzi chake, Bi Martha Kisandu pale kanisa la RC na baadae pale Maua Social Hall, Ubungo External.

Mwalimu huyo, mtaalamu wa lugha kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, alisindikizwa na wana Idara wenzake wa Idara ya Fasihi; Bw Emmanuel Lema na Bi Elizabeth Kweka na wengine kutoka Idara ya Lugha Za Kigeni na Isimu hapo UDSM.

Huku ukumbi ukiwa umependeza kweeli kweli na kukiwa na kiyoyozi cha haja hapo, wageni waalikwa walihakikishiwa burudani na wabobevu katika fani; McNdimbo Crew wakiwa na Kwayu Music Classic ikiongozwa na DJ Baby...ilikua ni noumar!!!

Wasukuma wakapata yao, wakristo wakapata yao, wazee wa zamani wakapoozwa na yao, vijana na enzi zao wakapata yao na hata vijana wa dot com wakarushwa ile mbayaaa. Watake nini tena. Kikwetukwetu, burudani ndio jadi yetu sieee; YOUR SATISFACTION IS OUR PASSION.

Songa nasi kimatukio kwa picha

Colours: Green na Orange


No comments: