Sunday, January 6, 2013

@ Kiramuu Hall, Peter Mahyenga Weds Victoria Moshi....

Mungu hupanga kila jambo kwa makusudi yake. Harusi hii ilipangwa! Ndoa hii ilipangwa! Shughuli hii ilipangwa na Mungu mwenyewe. Ingawa kabla ya siku hiyo, familia ya Bibi harusi ilipoteza ndugu wa karibu, bado Harusi ilifanyika kwa kua huu ni Mpango wa Mungu. Maharusi wakiingia kwa nderemo na huzuni ya mbaaali, walikaribishwa kwa shangwe na nderemo kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki. Furaha .

wakiwa wamefanana kama mapacha, Peter na Victoria kila ukiwaangalia wanakua wameshikana mikono yao. Kweli wanapendana hawa.

Kukamilisha furaha yao ya maisha ya ndoa , Pastor Stellah wa Glory of God Ministry, ambaye ni mama yake mdogo na Peter, aliwapa tiket ya ndege ya kwenda na kurudi Uingereza kwa ajili ya honeymoon na huku akiwa amewafanyia reservation kwa hoteli kwa wiki mbili. That was a thing!

Marafiki zao, wafanyakazi wa Tanesco, NBC na wahandisi wenzake na Peter wakaifanya shughuli ionekane ni ya kipekee kabisa katika ukumbi huo maarufu jijini Dar es Salaam.

Songa nasi hapa, japo kwa uchache wa picha na matukio.

Colours: Royal blue na White.

What a couple!!No comments: