Katika hali iliyodhihirika wazi kwamba hiyo siku ilisubiriwa kwa hamu kubwaa; kengele za kanisa la KKKT pale Ubungo zikagongwa, nyuma tu ya Ubungo Plaza, wakajongea kwa nyuso za furaha, wakafuatiwa na ndugu, jamaa na marafiki. Wakageuka nyuma na kushoto na kulia na bila kinyongo...kila aliyeulizwa lile swali maarufu, akajibu kwa bashasha na tabasamu la kutosha, YES I DO, katikati ya machozi ya furaha; James John Munuo na Bi Angela Lyimo became officially a man and his wife!!!
Hapo nderemo na vifijo zikavuma kutoka anga za kimataifa; Marangu mpaka kule Hai, Dodoma mpaka Songea kule kwa ugimbi! Ilikua raha iliyoje. Shughuli ikiwa imeandaliwa vyema na kuandalika. Wanakamati wakijipanga ipasavyo kuhudumia wageni waalikwa kwa tabasamu murua. Mambo ikawa hapo New Mawella Hall, moja ya kumbi za maana sana apo jijini Dar es Salaam.
Miongomi mwa marafiki wa karibu, walikuwapo members wa Kikundi cha The Fifteen Family, chini ya uongozi wake Mr Paschal Mwaja, wakaweka spices za kutosha na uhondo wa kulisakata sebene kwa style ya peke yake.
Dj Smol hakuwa na ajizi, akapanga ile mambo isochoshaga masikio na inayoweka makaa ya moto kwenye viti....basi weeeeee, kila anayekaa roho inamsuta! Akisimama anakutana na kideku e, hajakaa sawa anatokewa na shamukwale, akirudi huku analisakata kwaito..akageuka namna hii anakutana na " utajibeeba leooooo, umekula pesa zangu wee, utajibeba leooo" chezea McNdimbo wewe! Kweli YOUR SATISFACTION IS OUR ACHIEVEMENT.
Songa nasi hapa.
Colours: Pitch na Silver
|
Bw James munuo na mkewe kipenzi, bi Angela J. Munuo wakiwa na nyuso za furaha. Pembeni wakiwa na marafiki zao; Bw na Bi James Mrema, watoto; Kareen na Paschal |
|
Decor's |
|
Bw Gregory Ndimbo akiwa na shemeji yake |
|
Mrs McNdimbo |
|
Kwa raha zetu |
|
Dj Smol in da houe akimwaga mbigiriiii |
|
Karibuni wageni |
|
Wazazi |
|
Wazazi, Familia ya Munuo |
|
Wakwe, familia ya Lyimo |
|
Babies; Kareen Reuben na Paschal wakiingia na aunt ya bi Agnes Wajimila |
|
Ze Maids |
|
Mdau, kama kawaida akianza kupandisha mzuka |
|
James Munuo akiwa na mkewe Bi Angela James munuo wakiingia kwa sura za bashasha |
|
Hapo vipi wajemeeeni |
|
Mshikemshike |
|
15 Family: Bw Dennis Simba na mkewe |
|
15 Family: Bi Beatrice, Bi Pendo, Bi Saburi na Bi Tamara |
|
15 Family: Bw P. Mwaja (Mwenyekiti), Bw G. Machilika (Mhazini), Bw Kossey na Bw Denis Simba |
|
15 Family: Hapo vipi? |
|
Wazazi: Mzee Munuo akitangaza zawadi ya ng'ombe...kichagga zaidi |
|
Wakwe |
|
Kikundi cha kusaidiana cha kina Munuo |
|
Mdau akiwakaribisha Ze Wake wa Shemejiiz Group |
|
Wazazi wa James hapo mbele na nyuma ni McNdimbo, Borden Ndimbo, Gregory Ndimbo na wake zao |
|
Ze Brothers and Sisters |
|
Ze Kamati |
|
Mwenyekiti Msaidizi, Bw Mpande, Venance (Mzee wa Yanga Oyee) akihitimisha shughuli na wana kamati |
1 comment:
HONGERA SANA MY DEAR ,BLOG YAKO NZURI ,AMA KWELI KUTEMBEA KUONA MENGI..LEO NIMEAMUA KUTEMBELEA BLOGS NA NIKAKUTANA NA HII BLOG YAKO NA VILE VILE KUIPOST TO MY BLOG" HEADLINES NEWS! NI VIZURI MABLOGS KUJITANGAZA WENYEWE NAMI NIKIPATA NAFASI SASA NITAKUWA NA WEKA BLOGS HEADLINEWS KWA MY BLOG AND UTAKUWEPO NOW..MAANA NIMEIPENDA PIA,,ANYWAY ,,HAHARUSI WETU HONGERENI SANA NA MUNGU AILINDE NDOA YENU"
Post a Comment