Monday, April 8, 2013

Angella Lyimo is sent off at Cine Club

Huku Banana Zorro na B-Band, wakitumbuiza kwa rhumba na kwaitooz, raha ilioje kwa siku maalum ya kumuaga Angela mwana wa Lyimo. Hapo wachagga wote wakasahau habari za kujipanga na kuzungumza kuhusu mipango ya kutafuta mihela, wakaamua kujimwaga kwa burudani za haja mchanganyiko kutoka kwa B- Band na Dj Sammy. Hapa na pale zikiwa na break za maneno ya nasaha kutoka kwa wazazi.

Ilikua burudani na raha haswaa. James Munuo, mtanashati wa haja, akionekana dhahiri kua kiroho chamdunda na huku akiwa na kisebusebu, akaona mtoto Angela huyooo anaongozwa na chombezo la Nipe Macho Nione la Christina Shusho, akimtafuta mumewe hyo mtarajiwa ili akampe kampani wakati wa kula.

Uhondo ukanogeshwa na maids walipendeza kwa rangi safi ya harusi. Kwa kweli, big up imwendee big brother wa Angela- Humphrey- aliyefanya kila liwezekanalo, watu tusiboreke na tujisikie haswaa tunastahili kuwapo ndani ya ukumbi huo mdogo dogo kando ya Bahari ya Hindi.

Mdau, kama kawaida, nikawapa roho inapenda. Songa nasi;

Colours: Aqua Green na CreamNo comments: