Thursday, May 9, 2013

Police Officers' Mess: Emmanuel Zablon Mgonja weds Pretty

Wakiingia kwa style ile ya ku-march, The typical Seventh Day Adventist style, Mtanashat Emmanuel a.k.a Mzee wa Iglumut (walinguist wa UDSM 2006 class wanajua) na kipenzi chake- Pretty, best na neighbour wa ukweli, wamemeremeta ile mbayaa. Wimbo maalum ukasikika kwa masikio ya wageni waalikwa wale

'... Ni mbali tumetokaaa...na mahali tumefikaaa...ndio maana tunatambuaaa...kwamba wewe ni Ebenezer...nataka ndoa yangu, ijengwe juu yako baba, ndoa zilizojengwa juu yako Yahwe, hazivunjiki kamweeeee...'

Hapo wakasogeaa huku wakinong'onezana maneno ya furaha na Emma akimtambulisha mkewe Pretty kwa ndgu na marafiki zake kwa kuwapoint kwa macho...ilikua furaha sana ilioje. Walipofika katikati ya ukumbi, mtaalam Dj akawapa ile kitu ya kipare '..Hooooodi...' oh maammah! Wapare wakawa wapepagauwa....ni furaha kwa kwenda mbele. Maharusi wakabebwa juu kwa juu. Kweli mke kapata mume.

Siku hiyo hiyo ikawa ni maalum kwa mpwaye bwana harusi (mtoto wa dada yake), Loveness. Siku hiyo ilikua ndio birthday yake. Bila kinyongo, maharusi wakampa nafasi murua ya kukata keki yake na kuwalisha wazazi wake. Kweli hapo ilikua safiiiiii.

Songa nasi kwa picha

Colours; purple na hot pink

No comments: