"..Peji alikua mtundu sana wakati anasoma, lakini baada ya maelekezo ya kutosha na matunzo ya wazazi na walimu wake, alikuja kufahamu majukumu yake..ni jambo ya kumshukuru sana Mungu kwamba sasa Peji ni Mwalimu wa Chuo Kikuu..."
Hayo yalikua ni maneno ya mzazi wa Peji Lunyili akieleza wasifu wa binti yake uliorekodiwa na kurushwa moja kwa moja na wataalamu wa picha za mnato na video pale katika Ukumbi wa Mawela, Sinza siku ya kumuaga rasmi Peji Lazaro Lunyili.
Burudani ya ukweli ikiongozwa na jopo la McNdimbo Entertainment. Nyuma ya mashine akiwapo Dj Smol na mic ikiwa kwa mdau, basi kaazi ikawa imewakuta wenye nayo. Hapo ni hakuna kulala.
Wafanyakazi wenzake na Bi Harusi Mtarajiwa, wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Lugha za Kigeni na Isimu, Dr Rose Upor na wanataaluma wengine; Dr Abel Mrata, Dr Mapunda, Dr Shartielly na wengineo wakanogesha shughli ya mwana taaluma mwenzao. Hapo wakadhihirisha ule unaoonekana ni mkakati wa dhahiri wa kuhakikisha vijana wa Idara wasio na wenza wao wa maisha basi wanakuwapo nao. Yaani, baada ya kupata Bachelor degree na kuishi ki- bachela kwa muda wa kutosha, basi baada ya kupata degree ya ziada after Bachelor basi maisha ya kijamii pia yawe na ziada baada ya ubachela.....chezea wana Isimu wewe!
Tabasamu la kutosha na moyo wa upendo ukajidhirisha pale Bi Peji alipoamua kumvisha kiatu kipyaaaaa, mmewe mtarajiwa, Bw Goodluck Mshana. Hapo kila mtu alionekana kufurahishwa na tukio hilo adimu.
Songa nasi hapa kwa picha
Colours: Brown na Pink- Peach
!
No comments:
Post a Comment