Friday, August 2, 2013

Julianus to Esther! Utawapenda!!!!

Ooooooh oooooooh My God is gooood oooh!! Eeeeeeeeh.....eeehh eeeeehhh, my God is goood oooh!! Everything is double double!!! Shuka chini....chini tenaaaa....one two threee!!

Huo ndo ulikua mlipuko wa ndege wawili wapendanao kwa dhati; Bw Julianus Andrew Mambe na Bi Esther Brown Mwamafupa walipokua wakiingia kwa mbwembwe pale katika ukumbi maarufu jijini Dar es Salaam, Banora. Hapo wakiwa na uhakika wa kuishi pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha kama walivyoapa mbele ya waumini na mapadre wa Kanisa la Katoliki-Makuburi.

Huku wakisindikizwa kwa show ya hatari ya mabest friend; Emma, Eddy, Bruno, Lucas na mabinti kadhaa.na pembeni yao wapo wasimamizi wa ndoa na harusi hiyo; Bw Keneth Mvili na mkewe kipenzi, Praxeda.

Siku hiyo ambayo ilikua maalum pia kwa mdogo wake na Bwana harusi aitwaye Lilian John, aliyepata kipaimara na maharusi wakamlisha keki kama zawadi yao kwake.

DJ smol akiwapoteeza kabisa kwa uhondo wa wenyeji wote kutoka kule Ngoreme, serengeti na Kyela, Mbeya..za dini..kwaito....za zamaaaani na mijisebene na miduara...na weeeeee!! Bwana harusi akajikuta amenogewa na kuyarudi katikati ya wadau na huku akipigiwa makofi ya kutosha!! burudaani juu ya burudani ikiongozwa na sauti adimu ya dhahabu kutoka kwa mtanashati...Ze Blogger! YOUR SATISFACTION IS OUR PASSION

Songa nasi kwa picha

Colours: sivler na Navy Blue






























































































































No comments: