Monday, July 29, 2013

Stellah Mathias Mosha Pre Wedding Party...Classy!

Huku akizungukwa na mashosti wake wa A'Level, paleee Green Acres, akiwamo Winnie na Vanessa, mrembo huyo mwenye asili ya Kiraracha- Moshi, Bibi Stellah mwana wa Mosha,,aliingia ukumbini pale- King Palace, Sinza- kwa tabasaaam la ukweli na huku akishangiliwa kwa vifijo, nderemo na hoihoi kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki.

Akasindikizwa na kazi nzuri ya Christina Shusho, Nipe Macho Nionee, Bi arusi huyo akasogea na kumleta mbele ya kadamnasi na kumtambulisha rasmi mumewe mtarajiwa, Bw Nixon Biharabu. Kama vile haitoshi, Stellah akampatia zawadi mmewe yule mtarajiwa ya saa ya mkononi na kumvisha kimahaba. That was a thing!

Crew ya McNdimbo ikaja na ladha tofauti, ikiwa na ushiriano wa karibu na sound iliyokwenda shule kutoka kwao Kwayu Entertainment chini ya Dj Danny. Moto ulikua ni wa hataree wa muziki ule.

Katika kuleta uhondo wa kutosha, JJB Smart Boys wakachombeza na show yao safi ya Zunguka.
Kwa kweli, ile ilikua so goood of a special Night ya Stellah Mosha.

Songa nasi kwa picha hapa

Colours: Red na Gold


DJ Danny
No comments: