Katika kile kilichoonekana kama crew ya McNdimbo Entertainment basi itafunga kazi mwaka huu kwa kufanya shughuli zilizoongozana hapo katika ukumbi wa The Best Choice, Bw na Bi Kajenje walionekana kufungua pazia la mfululizo huo. Mara baada ya kuuacha ukapera, Bw Kajenje akiingia na mkewe ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili, walipata chaguo la wimbo mzuri kutoka kwa Bi harusi katika album yake mpya.
Kamati ya ulinzi ikiongozwa na mwanataaluma Emmanuel Kihongo na mdau katika sekta ya uvuvi na rasilimali za majini, Bw Humphrey Mahudi, ilisimama kidete kuhakikisha hakuna mtu anaingia pasipo tiketi ya siku hiyo ambayo ilikua ni kadi.
Ukumbi ukiwa umepambwa na kupambika ukawa na wageni waliochangamka ile mbaya, ukawekwa katikati ya burudiko la moyo kutoka katika crew yenye kuthamini burudani, McNdimbo Entertaimenment...Your Satisfaction is our Passion.
Songa nasi kwa picha hapa.
Colours; red na yellow
No comments:
Post a Comment