Wednesday, April 24, 2013

River Side, Dsm; William Komba weds Pendo Kayombo

Wakaonekana kama wanagalagala, wanalala mbele ya maharusi. Watu wakawashangaa. Watu wakajiuliza " inakuwaje hawa ndugu wanagalala mbele ya msafara wa maharusi?" hahahahahhha...kumbe hawakujua. Izo ni mila za watu wa Kusini mwa Tanzania; Wamatengo. Hapo walikua wakionesha ishara ya furaha na kukubali heshima waliyopata kwa watoto wao kufunga ndoa. Hapo ilikua "tuserebukeee aeeee aeeee...."

Bw William Komba na Bi Pendo Kayombo wakaingia hapo ukumbini wakiwa rasmi Mr & Mrs William Komba. Hiyo ilikua ni baada ya kutoa kiapo rasmi cha maisha; YES I DO, pale katika University Chaplaincy ya UDSM kwa Roman Catholic.

Vifijo na nderemo vikarindima hapo, majirani hao waliunganisha familia hizo mbili na kua ni ndugu haswaaa. Wakawa na nyuso za tabasamu mwanzo- mwisho. Hakika ilikua safiiii.

Kama kawaida, burudani kamilifu ikaongozwa kwa ustadi mkubwa na Mtaaluma Ze Blogger Mc na kuporomoshwa kwa ujuzi mbobevu na Dj Smol na kupambwa kwa utamu haswaaa na Vijana wa Zunguka The JJB; James, Jerry na Brown a.k.a The The Smart Boys. Hapo hakukua na kulala. Ukae kitini kwa nini sasa. Taka za zamani? Taka za Kisauzi? Taka za kisasa? Taka za kikabila? Taka za kidhungu? Weeeee....Burudani ndio Jadi yetu kukamilisha ule msisitizo wetu wa Mwaka Huu " Your Satisfaction is Our Achievement"

Songa nasi kwa picha hapa

Colours; Light Blue na Peach









































































No comments: