Thursday, June 20, 2013

It is Gilbert & Genoveeva a.k.a 'G wa G' at Urafiki, Dar es Salaam!!!

Kuna wakati unakua na mchumba ana jina limeanzia na 'Z' na huku la kwako limeanza na 'A'!!! Lakini kuna wenye bahati na kukuta majina yao yakiwa na herufi za kufanana. Ilikua ni furaha ya pekee kabisa pale ambapo maharusi wenye majina yanayoanza na herufu 'G' wakifunga ndoa na kuanza maisha matakatifu. Hawa si wengine ila ni mtanashati wa kichagga Gilbert mwana wa Shirima na Genoveeva.

Mambo yakaanzia paleeee St Martha Catholic Church, Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo watu walishuhudia zile vows za asili. Zikikamilisha penzi lililochipukia kama utani vile ila kumbe G akampata G wake pia.

Uhondo ukahamia ndani ya ukumbi uliofanyiwa renovation ya hatari na ukavutia haswaa na kupata kibali cha kuwapa haki yao The Gs kufanya shughuli yao pevu; Urafiki Social Hall.
Hapo, kama kawaida Stivangie Entertainment wakaleta muziki safi ulioshiba na nyuma ya mashine akawepo Dj Salim na mdau wenu nikawa pale katikati nikchombeza hapa na pale. Kama kawaida tukasuuza roho za waxhagga wale na kutoka na kiroho saaaafi...kwatu....kwatu! Tukatimiza uhondo wa half ya pili ya mwaka...YOUR SATISFACTION IS OUR PASSION!!

Songa nasi hapa kwa picha

Colours: baby yellow na purple


No comments: