Friday, July 26, 2013

Edwin Msambwa weds Agnes....what a Handsome Couple!

Katika kile kilichoonekana ni kampeni madhubuti inayoratibiwa kitaalamu haswaaa ya kuhakikisha vijana wote wa Idara ya Lugha za Kigeni na Isimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanapata wenzi wao wa maisha, sasa ikawa zamu na Mhadhiri Msaidizi Bw Edwin Msambwa pale alipofunga pingu za maisha na Bi Agnes.

Wakiwa na asili ya Nyanda za Juu Kusini; Njombe na Iringa Mjini, maharusi hao wakaingia ndani ya Ukumbi Murua wa Five Star kule Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Kwakua wote ni wapenzi wa Kwaito haswaaaa, basi wakaingia wakijimwayamwaya na buudani safi kutoka Afrika ya Kusini na bila ajizi Dj Smol akawaunganisha na mijikwaito ya haja.

Huku wakisindikizwa na wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi kutoka pale Nyerere Campus almaarufu kama Mlimani; Mwombeki, Njiro, Abel, Peji, Faraja na wengineo, wakajikuta wakitabasamu kuanzia mwanzo wa shughuli mpaka mwisho. Zaidi wakawepo wanataaluma wabobevu kuhakikisha wanakuwa mashuhuda wa tukio lile muhimu; Prof Rugemalira, Dr Kibogoya, Dr Muzale, Dr Mapunda na Dr Upor ambaye pamoja na kwamba alikua safarini siku hiyo alihakikisha hapitwi na tukio hilo mara tu baada ya kuwasili jijini.

Burudani mdio jafi yetu na watu ndio haswaa furaha yetu kuwapa burudani...

Songa nasi hapa

Colours; red na gold na greenNo comments: