Cha kwanza waweza kuona pale akitabasamu tu ni uleee mwanya...Mtoto wa Tanga huyo mwenye mwonekano wa kishombeshombe baab..LOURINE JIMMY. Ikafika wakati muafaka hapo ambapo aliamua ka moyo mkunjufu kuwaaga ndgu na jamaa ili akayaanze maisha ya ndoa takatifu na wake wa ukweli.
Wasambaa hao bila kushangaa wakajipanga vilivyo na kuamua kushirikisha ndugu, jamaa na marafiki ili kumuaga kipenzi wao katika ukumbi wa Lukolo, pale Tabata. Huku wakiwa na ucheshi wao wa asili na usongo wa haja wa kuburudika haswaaa na ngoma zao za asili bila ya kusahau maisha ya kiroho ya familia ile na kuburudika kwa nyimbo za injili na kumtukuza BWANA. Bila ajizi, crew nzima ya McNdimbo ikatoa ile raha ya ukweli na asili ya kukonga nyoyo za waalikwa. Hapo ni kata kiu mpaka kufikia malengo; YOUR SATISFACTION IS OUR PASSION....
Songa nasi kwa picha ...
Colours: Purple na Baby Yellow
No comments:
Post a Comment