Tuesday, October 29, 2013

Monday Israel weds Happiness Ruguga.....


Ilikua ni siku maalumu sana kwa kijana Monday Israel, aiyefunga safari kutoka masomoni kwake Cameroun na kuja moja kwa moja Bongoland na kufunga ndoa na rafiki yake wa ukweli, best na furaha ya moyo wake, Bi Happiness Ruguga.

Mambo yalianzia pale katika kanisa la  RC Kurasini na baadaye kujivinjari katika viunga vya Sabasaba Trade Fair kwa tafrija ya haja wakijimwaga na ndugu, jamaa na marafiki. Maharusi hao wana taaluma ya ualimu, bwana harusi ni Mkufunzi wa lugha ya Kifaransa katika Chuo Kikuu Kishiri cha Elimu, Dar es Salaam na mkewe akijiandaa kuajiriwa baada ya kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Arusha
Songa nasi katika picha
Colours: Purple na WhiteNo comments: