Tuesday, November 5, 2013

Pius Ntiga weds Neema @ Landmark Hotels...

Ilikua ni furaha sana kwa maharusi wale, Pius Ntiga na rafiki yake Bi Neema, mtoto wa kichagga. Shamrashamra zilianzia kuleee nyumbani kwa kaka yake na Bw Harusi, ambaye pia amekua ni mlezi wake tangu Enzi za sekondari Dr na Mrs Peter Mgosha. Baadaye wasukuma wale wakahaia katika kanisa la RC pale Msimbazi Centre. Hapo Mtanashati Pius akasahau mambo yake kutoka kule Uhuru FM na kumuhakikishia Neema wake kuwa wataishi milele mpaka kifo kitakapowatenganisha.
 
Utamu haukuishia hapo, uhondo halisi zikahamia paleeee Landmark Hotels chini ya Combination ya hatari ya McNdimbo na Dj Ndende kutoka Respect Djs (shereheyetu.blogspot.com). Hapo haikua kazi ngumu kuweka vichwa zaidi ya mia tatu katika usalama wa burudani kutoka mwanzo hadi mwisho.
 
Huku akiwapo Paschal Mwaja na kuongoza waleee watanashati kutoka The 15 Family, marafiki na majirani wa ukweli wa Dr & Mrs Peter Mgosha, Mlezi wa Bwana Harusi; Machilika, Simba, Nyambere, Karokola, Deo, Hamidu, Saburi, Tamara, Pendo, Faith, Mama Kamila na wengineo....na huku yupo Mamaaa Angel na Crew nzima ya Uhuru FM...moto uliwaka pale. Full maburudaaani ng'wanawane...zikaanza ndombolo ya solo, sebene, gospoooz, kwaito na taarab za ukweli...wataka nini tena banaaaaah
 
Songa nasi kwa picha hapa:

Picture na Video by LaserLooks Production (0763835478)
 
Rangi: Maroon na Gold
   
 


 
 
 

No comments: