Tuesday, November 12, 2013

Jumanne Weds Dyness....@ Mwenge Social Hall

Katika kanisa la RC, Tabata la Mt Anwarite, waili hawa wakala kiapo cha maisha. Wakiwa na tabasamu zao za asili, Mtanashati Jumanne na kipenzi chake wa siku nyingi na rafiki yake wa ukweli,Dyness, Wakasindikizwa na ndugu na marafiki zao hapo na kwa furaha isiyopomika, wawili hao wakaacha baba na mama zao na kuambatana pamoujar.
 
Uhondo ukanoga hapo na kama vile haukutosha, mambo ikahamia kwa ukumbi maarufu hapo Mwenge Dar es Salaam, waitwa Mwenge Social Hall-Kumbi Pacha na Mwik Social Hall wa pale Sinza. Hapo mambo yakawa baam baaam!!
 
Mtaalam wa fani, Dj Ndende akatulia hapo na chatter yake ya Respect DJs. Akawapagawisha na wakapagawaaaaa. Katikati, bila ajizi, sauti ya ukweli ikarinima ikiwakaribisha na kuwatabasamisha maharusi na wageni wengine hapo ndani, mwaanzo mpaka mwisho....heheiyaaa; mwendo mdundo...Tupooogo, bado tupooogo...tunachopata chocho mi na yeye tuuu, kiwe kidooogo, kikubwa ni majaliwa......" zikashuka za kikurya, za ijita, gospoooz...ikaja baak to baak...kitu ya I have been thinking about you...tukasogea mpaka DRC na kujiachia na mzee Koffi Antonio Olomide...tukaenda hadi Nigeria na kukutana na zileeeee za Personally!!! oh oh...tukavinjari mitaaya pwani ya mashariki ya Africa na kujiachia n taarabu na miduara...wataka nini tena!!
 
songa nasi hapa kwa picha
 
Rangi: Silver na Peach 
  

 
 

No comments: