Monday, December 10, 2012

Hilarious Moment! Cecil Bahati Njau weds Bi Anne Fibu Yunga @ Diamond Jubilee Hall...

Kuna wakati wa kila jambo... Kwa kweli, wakati huu ulikua wa furaha sana. A very hilarious moment. Mambo yakaanzia pale Kanisani. Kijana mtanashati, Bw Cecil Njau akatamka maneno mataaam ' YES I DO' na hapo akakamilisha ndoto yake ya siku nyiiingi ya kuishi na rafiki yake, jirani yake na kipenzi chake wa ukweli, Bi Anne Fibu Yunga mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo.

Wakiwa wamependeza na kusindikizwa na marafiki wao wa ukweli kutoka DRC, South Africa, Kenya, Dubai, USA, Moshi, Arusha na kwingineko, walijongea ukumbi maarufu katika ukanda huu wa Africa Mashariki na kati, Diamond Jubilee Hall. Hapo ikawa ni nderemo na vigelegele vya kutosha. Ni burudani kwa kwenda mbele... Kuanzia Kwaito, ndombolo mpaka Bongo flava. Yaani ni soo. Mdau a.k.a The Blogger nikiwachombeza kwa haja kabisa.

Songa nasi hapa kwa picha.

Colours: Green apple na Orange
No comments: