Monday, February 11, 2013

Jackson Isdory Mushi weds Victoria Shayo @ Mlimani City......

Wakiwa na nyuso za furaha kweli kweli, wakajongea altareni pale kanisa la RC la Mt Maximillian Kolbe, Mwenge D'salaam na kuzungumza maneno mazuuuri yaliyotarajiwa lakini yaliyofarijisha masikio na kukonga nyoyo zao "Yes I Do"; Bwana Jackson Isdory Mushi na Bi Victoria Shayo au Sia, wakawa rasmi Mr & Mrs Jackson Isdory Mushi.

Shamra shamra zikasonga na kuhamia paleeee Sam Nujoma Road, ndani ya viunga vya UDSM katika ukumbi maarufu ndani na nje ya Tanzania, Mlimani City. Hapo mdipo mtiti mzima wa kueleweka ulipojidhihirisha. Jackson, alikua na sapoti kubwa sana na ya kujuvunia kutoka kwa staff wenzie wa UDSM walioongozwa na VC, Prof Mukandala na Deputy wa Administration, Prof Mgaya.

Hapo ilikua ni burudani ya kukata na shoka; kichagga full! Wakaonja mbege, wakala ndafu...halafu miuzungu sasa...kitu cha cake! Mi- wine na miheinnken! baadaye tukajimwaga nadani ya buffet sita zilizopangwa saaaafi..nkakumbushia na kitu cha king fish! Basi weeee! Yaani watu zaidi ya mia saba wakala kwa muda mfupi kabisa; self service!

Mtaalamu, Dj Smol nyuma ya mashine akawapa ile roho inapenda....kwa poooz za sauti ya biashara na utanashati wa haja, Mdau wenu McNdimbo, nikawapa mchombezo wa 2013 haswaaa..... Wat a wedding this was!

Songa nasi hapa kwa picha...

Colours: Pink Rose, purple na silverTable Set up


Decor's


Ze cake


Wazazi; Dr na Mrs Mushi


Wakwe; Mr na Mrs Shayo


Maids na Groom's men


Wasimamizi
Mdau


Mbege time
Bwana Jackson na Mkewe Bi Victoria
Kitu ca Wema wa Mungu kwa kuwakaribisha maharusi
Bi Victoria


Hapo Jee
Ze kamati
Mwenyekiti Mr Minja akikaribisha wageni


Utambulisho


Champaign
VC wa UDSM, Prof Mukandala na Prof Mgaya na wake zao hapo
Kunywa baba


Nakupendaaje
Kunywa ma beib


Mmmmmwaaa


Cake tym
I love you
Mshikemshike


Mdau nikimsalimia Prof Mukandala, Makamu Mkuu wa chu Kikuu cha Dar es salaam
Nipo na kichwa changu, Dj Smol


Sisi ndo sisi


Mkwe


Wazazi


Ze ndafu


Prof na wewe onja ndafu
Bye bye


Executive Summary

No comments: